ILIPOISHIA…
Kilio cha Matrida
kilihuzunisha sana, alilia kwa uchungu kiasi cha sauti yake kuanza kuisha na
hatimaye akawa kama anakoroma tu, sauti haikuwa inatoka tena.
SONGA NAYO…
Baada ya mwezi kupita
familia ya Matrida ilikaa kikao kujadili maisha ya Matrida ataweza kulelewa na
nani, mama yake mdogo Matrida akasema “Matrida ni mwanangu ni mtoto wa dada
yangu mimi nitamlea Matrida na nitahakikisha anapata elimu sawa kama watoto
zangu wengine.”
Baada ya wanafamilia
kusema maneno mema na kumtakia mema,
Matrida alijisikia faraja katika moyo wake na kuwashukuru ndugu zake, tangu
siku hiyo Matrida alikua anaishi kwa mama yake mdogo.
Iliweza kupita miezi 3
baada ya kikao kile cha familia, Matrida alikua akishinda nyumbani peke yake ya
bila kwenda shule, ilipofika saa 1:40 usiku, familia ilikua mezani ikipata
chakula. Wakati wakiendelea kula chakula Matrida alikua akijiuliza maswali
mengi kuhusu maisha yake ya baadaye, aliomba kuongea kitu katika meza ile na
wakamruhusu kuongea:
“Nashukuru mama mdogo kwa
msaada wako ulio nipa wa kunilinda muda wote ila ile ahadi uliyoniahidi mbele
ya familia kuwa nitaendelea na masomo naona imeishia kati sikujua imefikia
wapi.”
Msaada mkubwa ambao
msichana Matrida aliwakua akiuhitaji kutoka kwa mama yake mdogo ni kumsomesha.
Baada ya madai ya Matrida
kutaka elimu, kumbe mama yake mdogo alikuwa hana mawazo wala nia ya kutaka
kumpeleka Matrida shule, akasimama huku akiwa amekunja ndita zake usoni na
kumwambia Matrida.
“Unajifanya umekuwa eti! Unataka kusoma …
hahahahaa sina uwezo wa kukusomesha na kama unataka kusoma subiri watoto wangu
wafike chuo ndio na wewe uanze darasa la kwanza.”
Matrida akamtazama mama
yake kisha akamwambia “Sasa kwa nini? Ulisema mbele ya familia kuwa utanilea
kama unavyowalea watoto wako wengine, na utanifanya niweze kupata elimu bora.”
Mama mdogo wa Matrida
alipoona mtoto Matrida anahitaji kujua mengi akamwambia “Sasa wewe unafikia
hatua ya kunijibu unavyotaka siyo… Mimi nimekuchukua wewe kwa sababu ya hii
nyumba, kama siyo hii nyumba usingeweza kukaa hapa na nina uwezo wa kuamua ukae
hapa au uondoke maana hii nyumba imeshakua yangu.”
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa