ILIPOISHIA…
Matrida alipoambiwa vile
akasema “ Mama muda wote nikae ndani tuuuuhh, aahh!!! Mimi nipo hapa nacheza” mara baba alikerekwa,
alimpiga kibao Matrida baada ya kumjibu vile mama yake na kumwambia.
ENDELEA NAYO…
“Matrida ni marufuku kumjibu mama hivyo tena,
inabidi umsikilize sawaaa?” Matrida aliitikia huku akilia. “Sawa baba,
sitorudia tena, kusema hivyo na naomba mama anisamehe.” Mama Matrida alimwambia
Matrida “Nimekusamehe mwanangu baba yako anahitaji uwe na tabia njema kama
watoto wengi, sawaa eeh mama yangu.”
Matrida alisema “ Asante
mama na asante baba kila kitu najifunza kupitia ninyi, nawapenda sana.”
Wakati Matrida alipokua
anafuta machozi kumbe yule njiwa alikua anamuona alivyokua analia, alikasirika
sana na alikunja uso kwa kuona rafiki yake amepigwa kibao na wale watu.
Wazazi wa Matrida
walipoanza safari yao ya kuelekea kazini
walipanda basi na wakati huuo Matrida alikua anarudi nyumbani na yule njiwa
aliondoka pale kwenye mti na kupaa angani.
Ilikuwa majira ya saa 7:15
mchana wakati Matrida akiwa sebuleni alisikia mtu akigonga mlango, Matrida
akawa mchangamfu kuharakisha kufungua mlango kwa kujua ni mama yake amerudi kwa
sababu siku zote yeye ndiye aliyekuwa anawahi kurudi nyumbani kabla ya baba
yako.
Cha ajabu siku hiyo
alipofungua akakutana uso kwa uso na shangazi yake akiwa analia sana na kusema
“ Mwanangu ajali imemuua baba… Matrida ajali imemuua mama…”
“Matrida weeee! Matrida
jamani mwanangu, weee, bado mdogo, ajali imeua baba na mama, jamani, jamani!”
Muda huohuo Matrida aliishiwa nguvu akaanza kulia.
Matrida alilia kwa uchungu
sana, uso wake ulijawa na kijasho chembamba huku machozi nayo yakimbubujika kwa
wingi huku akimlilia Mungu “Kwa nini umewachukua baba na mama yangu, basi
ungeniachia hata mmoja, Mungu kwa nini? unanichukulia tumaini langu la duniani,
sawa basi Mungu nichukue na mimi maana siwezi kuwa peke yangu” Matrida
alijihisi dunia nzima ameachwa peke yake.
Kilio cha Matrida
kilihuzunisha sana, alilia kwa uchungu kiasi cha sauti yake kuanza kuisha na
hatimaye akawa kama anakoroma tu, sauti haikuwa inatoka tena.
Nini kilifuatia, usikose ijumaa muda kama huu.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U