Wednesday, April 12, 2017

Published 4/12/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-50




NILIPOISHIA…

Nakumbuka kuna siku nilikuwa sina pesa ya kula kabisa, nhikiwa bado natafakali akaja mwanaume mmoja mbaye huwa anaishi jirani na ile gesti akaniambia…

ENDELEA…

 Yule mwanaume aliniambia niache kulialia, kama vipi nimpe penzi ili anipe pesa ya kula kwa usiku huo, nilifikiria sana, nilikuwa sina namna ikabidi nimpigie Bro G na kumuelezea ukweli ulivyo baada ya kuambiwa na yule mwanaume.

Usiku ule niliamua kumpigia simu Bro G, alisikitika sana akaniambia nisikubali kutoa penzi kwa sababu ya pesa, kwani stakuwa na furaha au sitahisi utamu wa penzi kwa sababu nitakuwa nimelazimisha kutokana na shida zangu.

Alinisihi sana kuhusu kujiingiza kwenye mahusiano kwa sababu ya shida zangu. Baada ya kunipa ushauri ambao uliniingia vizuri akilini mwangu, akaniambia “Kecho ninajitoa sana kwa ajili yako kwa sababu sitaki uishi katika maisha magmu uliyonayo, napigana hivi kwa ajili ya mwanao Gift ilimtoke hapo gesti, haina maana kuwa mimi sina shida, sina ndugu au jamaa zangu wenye shida au matatizo kama yako au kukuzidi, lakini nimekuswa kujitoa katika hilo.
 
“Hapa nilipo sina hela mkononi ila kwenye simu yangu kuna kama shilingi 40000, nakutumia shilingi 2500 kwa jili ya chakula, unaona kwa jinsi gani ambavyo najitoa kwako, mimi nabakiwa na 1500 wewe nakupa 2500, hivi una uhakika gani kama mimi nimekula au laha. Nafanya hivi ili kukusaidia, tafadhali sana, nitaumia sana kama nitakuja kugundua kuwa ulikuwa unanidanganya, unacheza na kuisumbua akili yangu.

“Kwani nikigundua hilo utakuwa umeuvunja moyo , moyo wangu kuwasaidia watu wengine ambao watakuja nyuma yako.”
Kweli alinitumia ile hela, nikanunua chakula siku ikaisha. Wakati huo G aliendelea kunipigania kimyakimya, pamoja na kufika pale gesti siku moja tu aliyokuja kunihoji na wenzake, hakuwahi kuja tena ila kila siku asubuhi, mchana na jioni au usiku ilikuwa ni lazima anijulie hali na kunipa mrejesho wa kile alichokifanya juu yangu.

Kuna siku alinipigia simu na kuniambia kuwa amezungumza na ofisa jamii wilaya ya kinondoni ili kuona kama wanaweza kunisaidia.

 Usikose kesho kujua nini alichoongea na ofisa jamii huyo?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit