MSANII wa Bongo Fleva,
Abubakar Katwila ‘Q-Chillah’ anayetamba na Wimbo wa Koku na Sungura,
Aprili 30, mwaka huu amejipanga kumtambulisha rasmi mpenzi wake anayefahamika
kwa jina la Lizy kwenye ‘event’ maalumu ya Miaka 15 ya Harakati za Q-Chillah.
Akizungumza na Show Biz
Xtra, Chillah alisema kuwa Lizy ni mwanamke ambaye amemvumilia sana katika
magumu yake, hivyo hana budi kumtambulisha rasmi kwenye umma, ikiwezekana kwa
kumvisha pete.
“Nimepita na Lizy kwenye
magumu mengi sana, lakini hakuwahi kuniacha, amekuwa mshauri wangu na rafiki
yangu, sasa ni muda muafaka wa kumtambulisha rasmi, aidha kwa kumvisha pete au
kitu kingine.