Monday, April 3, 2017

Published 4/03/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-42





NILIPOISHIA…

Nilianza kuhisi jambo kichwani mwangu, nikatafakari ni siku tatu sasa nimekaa pale, na chumba kila siku ni shilingi elfu saba. Nikiwa bado najiuliza mara ghafla nilisikia mlango ukigongwa, nikaamka na kujifunga vizuri kisha nikaulekea mlango ili kujua ni nani aliyekuwa anagonga na nini alichokuwa anakihitaji?

ENDELEA NAMI…


Aalikuwa muhudu wa ile gesti alikuwa amekuja kuulizia kuhusu hela ya malipo ya siku tatu nilizokaa, nilipigwa bumbuwazi nikagundua kuwa kuwa tayai nishaliwa tena, nilijitahidi kumweleza yule dada kuhusu jamaa kuniambia kuwa achumba alilipia lakini yule dada alikataa na kusema hakulipia wala hakuonana naye wakati anatoka.

 Tulivutana sana na yule dada hadi mwisho akamuita bosi wake, kuwa nimekataa kulipa siku tatu nilizokaa na sitaku kuondoka, niliumia sana kusema ukweli.

 Bosi alikuja nilimulezea mwanzo mwisho akanielewa lakini akanimbia ile ni biashara sina budi kulipia, kwahiyo akaniombe nijitahidi kutafuta pesa ya kumlipa hakuna na mengine zaidi ya pesa yake.
 
Nilirudi ndani nikaanza kujiuliza hadi machozi yakaanza kunitiririka, nilijiuliza sana ni nani na kwa namna gani anaweza kunisaidia kuweza kulipia hiyo pesa, sikuona kabisa. Niliendelea kulia kwa siku nzima, wakati huo mwanangu hakuwa na chakula na alikuwa analia sana kutoka na mguu wake kuuuma kwani ile 21000 niliyopewa nilikodi usafiri na kumpeleka mwanangu hospitali ambapo alinyooshwa mguu wake kwa hiyo alikuwa bado anamaumivu.

 Sikuwa na raha ,siku iliishia nikiwa sina kitu, yule dada  mhudumu alinionea huruma na kumnunulia mwanangu juisi ya embe ya mia 500 ndiyo akanywa, kisha akanipa uji wangu na mwanangu. Usiku ukwa umeingia hivyo. Hayo ndiyo yalikuwa maisha ya gesti wakati huo mwenye gesti aliendelea kuheshabu hela yake.

Baada ya kufikirisa sana nikajikuta nimepata wazo la mtu ambaye niliamini kuwa anaweza kunisaidia. Hivyo nilichofanya nikachukua kisimu change kilichokuwa chini ya mto kisha nikaanza kukibofya.

Je, Kecho anataka kumbofyea nani, na  ni kweli anayetaka kumbofyea atakuwa msaada kwake, usikose kesho muda kama huu.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.  0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit