Wednesday, April 19, 2017

Published 4/19/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-57



 
NILIPOISHIA…

Baada ya mchungaji kunisikiliza akadai itakuwa ni vyema kama watamuona mtu (Bro G) ambaye alinisaidia kuniunganisha na dada mtangazaji.


 siku hiyo nakumbuka nilisimamishwa mbele ya waumini.
ENDELEA…
Mchungaji alizungumza na waumini wake kisha akaomba nielezee mwenyewe kuhusu matatizo niliyonayo na kile inachokihitaji, niliona kama aibu fulani lakini nilikaza moyo nikaamua kufunguka kila kitu.

 Nilipokuwa nikizidi kusimulia kila mtu nilimuona akiwa ameshikwa na huzuni, waumini wakike walionekana kunongonezana na kuwalaumu wanaume kuwa ni watu wenye roho mbaya sana na wamekuwa chanzo cha wanawake wengi kutaabika.

 Halikadhalika hata wanaume nao walionekana kushikwa na imani dhidi ya mambo ambayo nilikutana nayo, hadi kufikia kuishi kwa dada mtangazaji ambaye ndiye haswa ameniunga nao.

 Baada ya kuzungumza kwa muda mrefu nilijikuta nikianza kulengwa na machozi kwani kuna mambo ambayo sikupenda kuyakumbuka wakati wa kusimulia kwa sababu yalikuwa yananikumbusha mbali sana.


Mchungaji alinisogelea na kuanza kunipigapiga begani kwa ishara ya kuninyamazisha, nililia kwa uchungu, basi wakaja wahudumu wa kanisani wakanitoa na kunipeleka pembeni na kuanza kuninyamazisha.

 Mchungaji alianza kuzungumza na waumini wake na kuwaeleza kuwa kuwa wao wamebarikiwa lakini ni vyema wakajua kuwa kuna watu wengine wanahitaji msaada mkubwa sana kutoka kwao, na wao ndiyo watu wanaotakiwa kuwasaidia. Kwani Yesu akuja duniani kwa ajili ya wale waliookoka au wenye uzima bali wasiookoka na wenye matatizo ili wapate kupona.

Mchungaji akaomba waumini wafanya harambee kwa ajili ya kunisaidia mimi na mtoto wangu. Msimamizi wa sadaka akaleta chombo cha sadaka na kuweka pale mbele, kisha waumini wakaanza kupita mbele na kuweka sadaka au harambee.

Nini kilifuatia, je, alipata  harambee ya kiasi gani?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U


      edit