Mimi niliolewa kwa ndoa kabisa na nikajaliwa kupata watoto watatu,
wawili wa kike na mmoja wa kiume.
Nimeishi kwenye ndoa na mume wangu kwa miaka 10 lakini ni miezi 8 tu
ndiyo niliyofurahia ndoa yangu baada ya hapo ni full mateso.
Ndoa imekuwa ni ya ugomvi kila kukicha, kila siku mimi ni wa kutukanwa,
kupigwa na kukejeliwa. Mwanaume hatulii kila siku ni kubadilisha tu wanawake,
kathubutu hata kutembea na mfanyakazi wa ndani. Inauma sana kwa kweli.
Nilivumilia kwa sababu ya watoto
wangu lakini mwisho wa siku nikachoka kwani mwanaume hanijali kama mkewe, hata
nikiumwa nijijue mwenyewe.
Niliamua kuondoka kwake na kurudi kwetu, kwa sasa mume wangu hana kazi, amekuwa
mtu wa kukaa tu nyumbani ila watoto nimemuachia. Baadaye aliniandikia talaka
kisha akachana vyeti vya ndoa. Ila mchungaji kasema ile talaka niliyopewa haina
nguvu ya kuvunja ndoa yetu.
Natamani niwe huru, niwe mbali na
mateso ya mwanaume huyu, sitaki na siko tayari kurudiana naye, naombeni ushauri
nifanyaje, nimelia, nimeteseka sana imetosha.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U