NILIPOISHIA…
Jioni iliingia hatimaye giza likaanza kutanda katika
anga ya Manzense na jiji zima kwa ujumla bila kupokea simu wala kumuona yule
kaka. Maumivu na kilio kilianza upya, nikimtazama mwanangu kapitiwa usingizi
hajui ninayoyapitia mama yake, hajui ninavyompigania apone mguu wake.
ENDELEA…
Alipotumiwa namba yangu na yule mtangazaji, alipoipiga
likatokea jina langu kwenye kioo cha simu yake, alijiuliza sana, kwa nini
Kecho, kwa nini mimi (yeye) nichaguliwe kumsaidia mwanamke yule yule ambaye
mara ya kwanza nilitaka kumsaidia ikashindikana.
Leo tena natumiwa namba ya mwanamake yuleyule, ni
lazima atakuwa anahitaji msaada kweli lakini dunia ina mambo sana, ni kuwa
makini kwa kila hatua
Yule kaka alinipigia simu asubuhi na mapema
kulipokucha na kuniomba samahani kwa kutokunipigia usiku jana yake kwa sababu ya dharura za hapa na
pale. Nilimwambia wala asijali kisha akaniuliza kama asubuhi ile angeweza kuja
kuniona nilikubali.
Kwa hatua
niliyokuwa nimefikia, nilimwomba yule kaka anisaidie kunikutanisha na vyombo
vya habari ili niweze kupata msaada niliona sina njia nyingine zaidi ya kuongea
na walimwengu kupitia mahgazeti, redio, runinga na vyombo vingine ili lengo
langu la kumsaidia mwanangu likamilike.
Yule kaka aliniaga na baaada ya muda alinipigia
nakunipa taarifa kuwa amefanikisha kupat watu wa habari hivyo niwe tayari na
wako njiani. Nilikubaliana naye.
Alifika yule kaka na kuanza kuongea na mhudumu wa gesti nadhani alifanya hivyo ili
kujiridhisha na kile nilichomwambia, mhudumu alimueleza kila kitu kuhusu
gharama ambazo nadaiwa, wakati huo haikuwa gharama ya siku tatu tena, siku
ziliongezeka.
Mhudumu alinigongea na kuniambia kuna wageni wangu
nikamwambia awaruhusu tu waingine ndani, waliingia vijana watatu, mmoja akiwa
na ndevu nyingi ambaye alikuwa ni kama kiongozi wao baadaye niligundua ni yule
kaka ambaye nilikuwa nawasiliana naye.
Kwanza yule
kaka alianza kwa kunipa pole na ushauri ambao ulianza kunijenga katika fikra
zangu, kisha akaniuliza maswali m kadha kwa kadha ikiwemo…
Mpenzi
msomaji usikose kujua nini kilifuatia baada ya msichana Kecho kufikiwa na watu
ambao aliamini kabisa kuwa wanaweza kumsaidia?
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U