Mambo Yanayokuzuia Kupata Furaha Ya Kweli Maishani Mwako.
Inaweza
kuonekana ni kitu cha kawaida lakini kuwa na furaha ya kweli na ya kudumu ni kitu
ambacho kinatafutwa sana na watu wengi. Ndio maana ukichunguza, harakati nyingi
za kutafuta maisha zinalenga hasa kupata furaha.
Hata
hivyo pamoja na watu wengi kuitafuta furaha sana, lakini bado wengi pia
wanaendelea kugubikwa na huzuni nikiwa na maana ni watu ambao wanaishi
maisha
hayana furaha sana kwa sehemu kubwa.
Je, hebu
tujiulize ni mambo gani ambayo yanasababisha mtu mmoja akawa na furaha au
mwingine akaikosa furaha? Majibu ya maswali haya utayapata kwenye makala haya.
Kikubwa fuatana nasi tuweze kujifunza pamoja.
1. Kufanya kazi usiyoipenda.
Ipo
asilima kubwa sana ya watu ambao wanafanya kazi ambazo mara nyingi wanakuwa
hawazipendi sana. Kwa lugha rahisi wanakuwa ni watu wanafanya kazi ambazo
hawazifurahii, kikubwa kwao inakuwa ni kutaka kuingiza kipato tu basi.
Kama
unafanya kazi ya namna hii ambayo huifurahii, lakini lengo lako ni kuingiza
kipato basi elewa unabeba moja ya kitu
ambacho kinakuzuia kupata furaha katika maisha yako kwa namna moja au nyingine.
Watu
wote wenye mafanikio wanafanya vile vitu ambavyo wanavipenda kutoka moyoni
mwao. Kama hufanyi kitu unachokipenda, leo hii ukianza kufanya kitu ambacho
unakipenda, uwe na uhakika utaanza kujenga furaha yako.
2. Kujilinganisha na wengine.
Ni tabia
ya wengi wetu tangu tukiwa watoto wadogo kutaka kujilinganisha na watu wengine.
Kwa bahati mbaya tabia hii imekua ikikua hadi kuweza kufikia ukubwani na kwa
wengi wetu tena tumekuwa tukiindeleza pasipo hata kujua.
Mara
nyingi tumekuwa tukijilinganisha katika vipato vyetu, tumekuwa tukijilinganisha
katika mavazi na mambo mengine chungu nzima. Hivyo, kutokana na kujilinganisha
huko sana imekuwa ikipelekea sisi kukosa furaha.
Kikawaida
huwezi kuwa na furaha kama kila wakati unajilinganisha na wengine. Maisha na
furaha yako inabaki kuwa yako kama kweli unaishi wewe kama wewe. Kujilinganisha
na wegine ni sawa na kutengeneza mazingira ya kupoteza furaha yako moja kwa moja.
3. Kuogopa mambo mengi.
Ni asili
ya binadamu kuwa na hali fulani ya woga. Kuna wakati tunakuwa tunaogopa mambo
yanayotudhuru au kuna wakati tunakuwa tunaogopa kujiingiza katika jambo fulani ,
mathalani hata uthubutu wa kufanya kitu fulani.
Sasa
inapotokea unakuwa ni mtu wa kuogopa sana mambo mengi na kila wakati, hiyo
inakuwa ni changamoto mojawapo ambayo inakuzuia moja kwa moja wewe kuweza
kupata furaha ya kweli.
Furaha
ya kweli mara nyingi inapatikana hasa kwa wewe unapokuwa huru na mambo yako. Unapokuwa
huru huna hofu ya mambo mengi na kuishi kwa kujiamini, hapo ndipo unakuwa na
furaha ya kweli.
4. Kuishi wakati uliopita.
Kuna
watu ambao wengi wetu badala ya kuishi sasa, hujikuta ni watu wa kuishi kwa
kukumbuka sana matukio mengi yaliyopita. Kama unaishi hivi kwa kukumbuka mambo
mengi yaliyopita na ambayo yalikuumiza kwa namna moja au nyingine uwe na
uhakika, furaha yako utaipoteza.
Kujenga
furaha ya kweli unatakiwa kuishi sasa na wala si kesho. Fanya mambo yako kwa
kuzingatia sana sasa. Watu wngi wenye mafanikio na furaha ya kweli wanaishi sasa
na kusahau mambo mengi yaliyopita.
Kumbuka
wewe ndiye unayewajibika na kutengeneza furaha ya kweli katika maisha yako. Zingatia
mambo hayo yanayokuzuia kupata furaha ya kweli.
Uwe
na usiku mwema na kila kheri katika kufikia mafanikio makubwa.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U