ILIPOISHIA…
Mama mdogo wa Matrida
alipoona mtoto Matrida anahitaji kujua mengi akamwambia “Sasa wewe unafikia
hatua ya kunijibu unavyotaka siyo… Mimi nimekuchukua wewe kwa sababu ya hii
nyumba, kama siyo hii nyumba usingeweza kukaa hapa na nina uwezo wa kuamua ukae
hapa au uondoke maana hii nyumba imeshakua yangu.”
SONGA NAYO…
Kumbe mama mdogo alikubali
kukaa nakuishi na Matrida sababu ya nyumba ambayo aliacha baba na mama mzazi wa
Matrida.
Matrida alivyosikia hivyo
machozi yakawa yanamtoka, alijikuta akiongea maneno ya uchungu sana huku akilia
“ Siku moja baba na mama yangu watarudi, najua Mungu atanirudishia tu na
nitawaambia yote uliyonifanyia, we’ utaona tu ma mdogo.”
Masikini Matrida alikua na
matumaini ya kuwa siku moja wazazi wake watarudi tena, ilikua ni usiku wa saa
4:30 ndipo Matrida alielekea chumbani kwake ambako hakuwa na tepe la usingizi
bali aliendelea kulia kwa uchungu nsana, hakutamani tena kuishi. Aliona dunia
chungu, dunia iliyojaa kila aina ya udhalimu. Hakika DUNIA KATILI.
MATRIDA ni mtoto mwenye
umri wa miaka 6 tu lakini Mungu alimjalia akili za kipekee sana. Wakati Matrida
akizidi kulia chumbani kwake, mara
akamuona yule njiwa mwenye rangi ya bluu, kijani na nyeupe akiwa
dirishani akimtazama Matrida akiwa analia.
Matrida alipomuona yule
njiwa alifuta machozi kisha akasema “Ni wewe rafiki yangu umekuja?” Matrida
alitoka nje na kumfuata yule njiwa na akambeba kisha akaingia naye ndani bila
mtu yeyote kumuona.
Matrida alipoingia naye chumbani akaanza
kumuuliza yule njiwa “Umekuja saa ngapi dirishani?” Njiwa, kimya.
“Mbona siku ile uliondoka
ghafla sana?” Njiwa, kimya.
“Mmmmhh mbona uongei sasa
rafiki yangu au nimekuudhi?”
Yule ndege alisema “Kwa
nini, unalia?” Matrida alishangaa kwa swali hilo akamjibu.
“Rafiki yangu mwenzako sasa hivi sina baba
wala sina mama wamekufa wote, ndiyo nilikua nalia.” Yule njiwa ndege akauliza
tena “ Matrida kwa nini, unalia?”
Matrida akamshangaa yule
ndege baada ya kumuona akiwa amenuna huku sura yake ikionekana amedhamilia kujua
kitu.
Matrida akamwambia, “haya
basi rafiki yangu ntakuambia ila usije ukamwambia mtu niahidi.”
Yule njiwa akauliza kwa
mara ya 3, “ Matrida niambie kwa nini unalia?” Matrida akaanza kumwambia yule
njiwa, “sawa ntakuambia… Mama na baba baada ya kufariki dunia, mama yangu mdogo
aliniahidi kuwa atanilea sawa na watoto wake lakini kumbe nia yake ilikuwa
akabidhiwe nyumba yetu. Nilipomuuliza kuhusu kunisomesha akachukia na kuniambia
kuwa nijiandae kuondoka na hii nyumba eti tayari imekua ya kwake.”
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U