Sunday, April 16, 2017

Published 4/16/2017 12:00:00 AM by

MAHARI NIMETOA, GARI NIMENUNUA LAKINI NATUKANWA VIBAYA!



MAHARI NIMETOA, GARI NIMENUNUA LAKINI NATUKANWA VIBAYA!

Mimi ni mfanyabiashara, kabla sijaona nilibahatika kupata mtoto na mwanamke mwingine, nilipoamua kuoa nilimwambia mwenzangu kuwa nina mtoto.

Nilimwambia suala la mtoto tukiwa bado hatujaoana kwa kujua kuwa atakuwa na mapenzi na mtoto wangu. Kwani kwenye uhusiano wa kawaida tumedumu kwa miaka 4 na kwenye ndoa sasa ni miaka miwili.

Lakini nilipofunga naye ndoa ndiyo akaonesha kabisa makucha yake, mtoto wangu akaawa hampendi. Nilivumilia nikamnunulia gari kwa ajili ya kwendea kazini kwake, na kila mwisho wa mwezi namuwekea mafuta ya hela nyingi tu.

Hataki kuulizwa kitu anataka kupanga yeye kiwe kizuri au kibaya, asipangiwe mda wa kwenda kazini wala wa kurudi yani kwa ufupi hataki kuulizwa chochote.

ukimuuliza kitu ndiyo chanzo cha ugomvi  na ugomvi wake ni wa siku tatu, unikaripia kwa majibu mabaya ya kiburi, sijazoeaga kumjibu ila akishaamua kunikalipia atakavyo. Please please ninaombeni ushauri nifanyeje?



Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U                      

      edit