Tuesday, April 4, 2017

Published 4/04/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-43





NILIPOISHIA...

Usiku kucha nilikuwa nafikiria ni kwa namna gani ninaweza kupata msaada, baada ya kuwaza sana hatimaye nilipata wazo ambalo niliamini kuwa linaweza kunisaidia.

ENDELEA NAMI...

Nilimkumbuka yule mkaka ambaye ni mtangazaji wa redio ambaye aliniunganisha na Jamaa mmoja ambaye alijaribu kunitafutia msaada kwa Madam Rita ila ikashindikana.

Nilimpigia simu yule mtangazaji na kumueleza kuwa NIMETELEKEZWA GESTI NA MWANAUME NIKIWA NA MTOTO WANGU, alisikitika sana akaniambia ngoja ajaribu kuangalia ni kwa namna gani anaweza kunisaidia kwani kipindi hicho yeye alikuwa nje ya mkoa.


Alichofanya ni kuniunganisha na yule kama ambaye aliwahi kutaka kunisaidia. Mtangazaji alinitumia namba ya yule mkaka nilipoiandika kwenye simu yangu nikashangaa kwani namba nilikuwa nayo.

Nikashusha pumzi na kujiuliza huyu kaka kuna wakati alitaka kunisaidia ili ilishindikana kweli atanipa msaada tena. Niliendelea kujiuliza pale kitandani, nikiwa na mtoto wangu.

Ni takribani siku zote nilikuwa nakula kwa kuungaunga kwa kupewa chochote na wasamaria wema kwani sikuwa na namna ya kupata pesa.

Mwanangu mkuu uliendelea kumsumbua kwani ulikuwa unamuwasha sana kwa sababu alikuwa amenyooshwa na kufungwa POP.




Hakuwa anapata chakula cha kutosha, sikuwa naweza kumnyonyesha kwa sababu maziwa hayakuwa yanatoka kwa sababu sikuwa napata chakula kinachozalisha maziwa kwa wingi.

Ilifika sehemu mtoto wangu nikawa namnyweshwa tu juisi ya mia tano siku inaisha. Nilimuona kama anaanza kukonda sana, niliumia sana moyoni mwangu, nilikumbuka maisha yangu ya awali, niliyokuwa nayo, nilivyolaghaiwa na Maiko nikampa penzi.

Niliendelea kuwaza na kuwazua mwisho nikaamua tu kumpigia simu yule kaka ambaye namba  yake nimepewea na mtangazaji wa redio.

Nilipiga sana simu yake ikawa inaita tu. Mwisho nikakata tamaa. Nikaamua kupotezea tu.

Je, nini kilifuatia baada ya kupiga simu ya mtu anayeamini kuwa anaweza kumsaidia lakini hapokei simu?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit