Saturday, April 29, 2017

Published 4/29/2017 04:31:00 PM by

MWENYE DHAMILA HASHINDWI WALA HAKATI TAMAA!


Tumshukuru Mungu kwa kutupa nafasi ya kuweza kuiona Jumamosi hii, kuna wengine walipenda lakini ikashindikana. Kuna magumu mengi ambayo tunayapitia kama wanadamu lakini kamwe yasitukatishe tamaa kama kweli tutamshirikisha Mungu.

Kufikia ndoto au malengo ya jambo fulani si jambo la kitoto au kawaida, ni jambo ambalo linapaswa liwe na msukumo wa kutoka ndani ya mtu mwenyewe.

Lazima ujiulize kwa nini unakataa tamaa au unataka kushindwa kwenye dhamila yako ya muda mrefu? Kwa mtu mwenye nia, dhamila na jambo fulani ambalo analipenda na kuliamini kutoka moyoni mwake basi kamwe hawezi kukata tamaa vipi hata kama atatukanwa, ataonekana mjinga lakini kwa kuwa yeye anaamini katika ndoto zake basi atasimamia ukweli wa mawazo yake.

Kwa mwenye dhamila ya kweli huwa hashindwi wala hakati tamaa bila kujali ugumu na changamoto anazokutana nazo.

Kama unashindwa au kufikiria kukata tamaa basi inawezekana hilo jambo au kitu ulichotaka kukifanya siyo kile ambacho unastahili kukifanya bali hicho ni kama "umekibaka" si lile ambalo ulizaliwa kulifanya au si lile ambalo unalipenda kwa moyo mmoja.




Ukitaka kufanya jambo angalia kwanza ni jambo lipi unalolipenda na kuliweza kulifanya? Hata kama ni usiku wa manane uko tayari kuamka na kulifanya jambo hilo.

Wengi wanaokuwa wanafeli ni wale ambao wanakuwa wanabaka jambo, pengine kasikia tu kuna mtu aliwahi kulifanya ana akafanikiwa na yeye anaamua kulichukilia juu kwa juu.

Jambo ambalo linaweza kukufanya ukafanikiwa ni lile ambalo una dhamila ya kweli pekee ambalo hata kama litachukua muda mrefu lakini ipo siku utalifanikisha. Hata kama unakutana na changamoto nyingi kiasi gani lakini moyoni mwako unaamini utalitimiza siku moja.
Usikose mada nyingine.


Kwa Ushauri Wa Uhusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na:M&U
      edit