NILIPOISHIA…
G alikubali na
kumuahidi yule dada kuwa watakuwa bega kwa bega hadi mwisho wa suala langu.
Dada mtangazaji alikubaliana na G na kumuahidi anipeleke siku inayofuatia.
SONGA NAYO…
Bro G
alinipigia simu na kunipa muongozo kwa kile alichokisema yule mdada mtangazaji,
kuwa yuko tayari kunisaidia, nilifurahi sana moyoni mwangu hata kabla sijawa na
uhakika ili niliamini G alikuwa kishakamilisha kila kitu.
Usiku wa siku
hiyo kuna wakati nilitamani uwahi
kukucha kwa sababu niliona ni kama usiku umekuwa mnene sana, nikiamini mwisho
dada mtangazaji anaweza kughairi maamuzi yake.
G alinitumia
nauli kisha akanielekeza mahali pa kumkuta ambapo ilikuwa ni ofisini kwao,
nikiwa mimi, mwanangu na kimkoba kidogo cha kizushi huku mkononi nikiwa na
kimfuko cha Rambo kikiwa na nguo za mwanangu.
Nilifika na
kumuuliza G kwa mlinzi aliyekuwepo zamu, nilimuona G na kufurahi alinipokea
vizuri na kuniagizia chakula, kisha yeye akaingia ofisi na kumalizia kazi.
Niliendelea
kumsubiri G kiasi kwamba nilichoka, nilitamani hata niondoke kisha nitarudi
baadaye lakini sikujua niende wapi kwa sababu sikuwa na pesa, sikuwa nafahamu
ni wapi nitaenda hivyo nikajikuna nikiwa mpole na kuendelea kumsubiria.
Baada ya saa
moja kuisha G alitoka ofisini na kujua nilipokuwa kisha akanipa pole kwa
kunicheleweshwa kwa sababu ya majukumu aliyokuwa nayo ndani.
Tulianza safari
ya kuelekea ofisini kwa dada mtangazaji, tulifika mapolezi tukapokelewa na
kuambiwa kuwa dada mtangazaji alikuwa kwenye kipindi hivyo tumsubiri.
Je, nini kilifuata baada ya dada
mtangazaji kutoka kwwenye kipindi?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba,
Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na
M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U