NILIPOISHIA…
Nilipiga sana simu yake ikawa inaita tu. Mwisho
nikakata tamaa. Nikaamua kupotezea tu.
ENDELEA NAYO…
Niliamua kupotezea na kuiweka simu kwenye kimeza
kidogo kilichopo kwenye chumba cha gesti. Nilianza kulia huku nikitafakari lini
na mimi nitapumzika maisha ya shida hapa duniani, lini mwanangu Gifti atapata
msaada wa matibabu ya mguu wake.
Nililia kimyakimya hadi nikapitiwa na usingizi,
nilishtushwa na mtetemo wa simu yangu ambayo ilionekana iliita sana kwani
niliona kulikuwa na Missed Calls zaidi ya 5 na zote zikiwa ni ya yule mkaka.
Sikuamini
niliamua kupokea ile simu na kuanza kujielezea, kabla hata sijaanza kueleza
vizuri yule kaka alinikatikza na kuniambia kuwa kila kitu anakifahamu, hivyo
nimpe maelezo kwa njia ya mswali, akaanza kuniuliza mswali mbalimbali.
Nikamjibu kisha akaniambia nivumilie hadi jioni
atakapopata muda kwani kwa wakati ule alikuwa anatoka kwenye majukumu mengine
hivyo hatoweza kufika kwangu bila kupitia ofisini kwake kisha ajipange kuja
kuzungumza na mimi.
Nilimnung’unikia sana yule kaka kuwa ajitahidi
basi aje kunisaidia kwani ninazidi kuadhirika pale gesti. Alikubaliana na mimi
na kumuoamba nimwamini. Kwa kuwa niliona napotezea muda nilimkubaliana kishingo
upande lakini kwa shida zilizokuwa zimenijaa niliona kama ananizingua tu na
kunichelewesha kunisaidia.
Kwa kifupi
nilichoka maisha ya kuzozana na wahudumu wa gesti ile, ilifika kipindi waliponidai niligeuka mbogoa
na kuogea kwa kiburi kabisa kuwa sina pa kwenda na mtoto mdogo niliyenaye.
Sitaki kutoka wafanye wanavyoweza kufanya, kusema ukweli nilijua kabisa kuwa
navunja utaratibu wao lakini sikuwa na namna ilinibidi nijifanye mkorofi
nisiytesikia wala kuambiwa chochote isipokuwa ni kutaka msaada
Basi waliniacha lakini wakanipa muda kuwa kufikia siku
fulani niwe nimewapa pesa zao.
Jioni iliingia hatimaye giza likaanza kutanda katika
anga ya Manzense na jiji zima kwa ujumla bila kupokea simu wala kumuona yule
kaka. Maumivu na kilio kilianza upya, nikimtazama mwanangu kapitiwa usingizi
hajui ninayoyapitia mama yake, hajui ninavyompigania apone mguu wake.
Je, nini kilifuata baada ya yule kaka kutokutokea?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba,
Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na
M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U