NILIPOISHIA…
Tulianza safari
ya kuelekea ofisini kwa dada mtangazaji, tulifika mapokezi tukapokelewa na
kuambiwa kuwa dada mtangazaji alikuwa kwenye kipindi hivyo tumsubiri.
ENDELEA…
Dada mtangazaji alitoka kwenye kipindi na kuja kutusalimia tulipokuwa tumekaa kisha akaomba muda kidogo akaingia ofisini na klisha kurudi tena kwetu.
Sasa G nimejaribu kufikiria nikaona ni vyema
pia kuwashirikisha wafanyakazi wenzangu hapa kazini kuhusu tatizo la dada
Kecho, pengine wanaweza kuwa na msaada mkubwa zaidi yetu.
G
alininong’oneza jambo kisha akamwambia dada mtangazaji, sawa haina shida. Basi
tuliingia ofisini na kuwakuta wanaume wawili na wanawake wawili.
G aliamua
kuelezea kwa ufupi kisha akatoa nafasi ya wao kuniuliza maswali, niliulizwa
maswali na kuyajibu nikisaidiana na G.
Baada ya kumaliza maswali, basi kila mtu
alitoa nasaha zake na kunishauri ni vyema nikakae kwa dada mtangazaji wakati
wao wanaendelea kuangalia namna ya
kunisaidia zaidi.
Nilikaa pale kwa muda kwa ajili ya kumsubiri
dada mtangazaji ili amalize majukumu yake. Alimaliza na kuanza safari ya
kuelekea kwao Kimara.
Tukiwa njiani,
G aliendelea kunishauri na kunisisitiza kuwa huku ninakokwenda nikawe mvumilivu
sana kwani mtu nitakaenda kuishi naye si ndugu yangu bali kajitolea kunisaidia,
hivyo napaswa kuvumilia na kufuata kile anachokitaka. Nijaribu kumsoma kuwa ni
mtu wa aina gani na mimi niende naye.
Tulipofika
kituoni G aliomba kutupiga picha ya kumbukumbu tukiwa kituoni hapo, mimi, dada
mtangazaji na mkaka mmoja ambaye alikuwa anatangaza na dada yule.
Je, nili kilifuatia?
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U