NILIPOISHIA…
M&U ilianzisha group
mbalimbali za Mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa ajili ya ushauri basi G
aliamua kutumia group hilo kufikisha ujumbe wa Kecho kwa watu ambao amekuwa
akishirikiana nao. Alifikiria sana kitu cha kufanya juu ya Kecho mwisho akaona
ni vyema kama ataadika kitu fulani.
ENDELEA…
Aliamua kuandika historia
yangu kwa ufupi kuhusu niliyoyapitia kichwa cha habari cha mada hiyo kikiwa
“Mama, Mwanaye Watelekezwa Gesti” kisha akaelezea kuhusu mahitaji ambayo
natakiwa kuyapata katika siku ambazo nitakuwa pale gesti lakini ni pamoja na
kuhitaji mtoto wangu atibiwe mguu.
Siku ya kwanza tangu G
afike iliisha nikiwa ni kama sina shida, ni kama nilikuwa nimefarijika, kwa
ushauri wake lakini kwa pesa kidogo ambayo aliniachia kwa sababu ya matumizi ya
hapa na pale.
Wakati huo miliki wa gesti
aliendelea kuhesabu idad za siku ambazo nimekaa kwake na kudai gharama ya mimi
kuwapo pale.
G . alifanikiwa kunitumia
pesa ya kula na nyingine ya kulipia chumba kwa siku zile nilizokaa , huku
kichwani kwake akiwa anajiuliza ni wapi atanipelekea ili nipate hifadhi ya
muda, kuepusha gharama za gesti.
Basi alipowashirikisha Group la M&U
walinionea huruma sana wakaamua kujichangachanga ikapatikiana kama shilingi
60000 kama sijakosea, ambayo G alikuwa ananitumia kwa ajili ya gesti na
matumizi mengine.
Niwashukuru sana wana
M&U popote pale walipo, walionisaidia kunichangia na hata ambao
hawakuchanga ila walionesha kuguswa na jambo langu ila hawakuwa na uwezo kwa
wakati huo.
Nilitamani japo kuwaona
M&U wote lakini haikuwezekana ila
mchango wao ulifika kwa kuwakilisha na Bro G. Mungu awabariki sana ila
kujiuza ndiyo hatua niliyofikiria nikiamini pengine ninaweza kujinuthuru kwenye
ugumu wa maisha nilionao.
Nililipa pesa ya gesti na nyingine nikabakiza
kidogo kwa ajili ya matumizi ya hapa na pale. Siku zikazidi kusonga nikiwa pale
gesti, pesa ya M&U ikiendelea kutumika. Wakati mwingine G akiladhimika
kutoa pesa yake mfukoni kwa ajili yangu, inawezekana ikawa siyo pesa kubwa sana
lakini ni ndogo yenye thamani.
Nakumbuka kuna siku nilikuwa sina pesa ya kula
kabisa, nhikiwa bado natafakali akaja mwanaume mmoja mbaye huwa anaishi jirani
na ile gesti akaniambia…
Mpenzi msomaji unajua nini ambacho aliniambia yule
mwanaume? Usikose kesho.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U