NILIPOISHIA…
Mchungaji
akaomba waumini wafanya harambee kwa ajili ya kunisaidia mimi na mtoto wangu.
Msimamizi wa sadaka akaleta chombo cha sadaka na kuweka pale mbele, kisha
waumini wakaanza kupita mbele na kuweka sadaka au harambee.
ENDELEA…
Mchungaji alianzisha ile harambee na waumini wengine
wakanza kuchangia pesa kwa ajili ya matibabu ya mtoto wangu. Mwitikio wa
waumini wale katika kuchanga ulikuwa mkubwa sana, nilikuwa kama siamini kwa
kile kinachoendelea lakini mwisho niliamini kuwa nimeuoana mkono wa Bwana
ukitenda maajabu.
Baada ya ile harambee pesa ikahesabiwa na baadhi ya
wahudumu wa kanisa lile na wakaja mbele ya waumini kutangaza kuwa wamepata
shilingi lakini moja na elfu thelathini, nilifurahi sana.
Mchungaji akarudia kutangaza kiwango kile cha pesa
kisha akaniambiwa kuwa pesa ile si yangu bali ya kumsaidia kumuuguza na
kuunyoosha mguu wa mwanangu.
“Kesho mimi na waumini wangu tumekuchangia pesa hii
kwa ajili ya matibabu ya mwanao, hivyo moja kwa moja kuna muumini ambaye kanisa
litamteua kuungana nawe katika kuhakikisha mnaenda wote CCBRT ili kumaptia
mtoto huyu huduma. Waumini wanahitaji kujiridhisha kwa pesa ambayo
wameichanga.”
Nilikubalina na mchungaji, kisha tukaendelea na ibada,
majira ya saa 8 mchana ibada ikawa imeisha, mchungaji akaniita hadi ofisini
kwake na kisha kumuita na yule dada mtangazaji na kumwambia kuhusu mchango ule
lakini hawawezi kunikabidhi mimi mwenyewe hadi waonane na Bro G kujiridhisha
kama kweli nina shida au nataka kuwatapeli.
Dada mtangazaji na mimi tulikubalina na mchungaji
kuhusu kumtafuta G. dada mtangazaji alipotoka kanisani akampigia G moja kwa
moja na kumuelezea kuhusu suala hilo.
Je,
kutokana na majukumu ya G atapata muda wa kuja kuonana na mchungaji huyo?
Usikose
kesho muda kama huu.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U