NILIPOISHIA…
Nilikubalina na mchungaji, kisha tukaendelea na ibada,
majira ya saa 8 mchana ibada ikawa imeisha, mchungaji akaniita hadi ofisini
kwake na kisha kumuita na yule dada mtangazaji na kumwambia kuhusu mchango ule
lakini hawawezi kunikabidhi mimi mwenyewe hadi waonane na Bro G kujiridhisha
kama kweli nina shida au nataka kuwatapeli.
Bro G alikubali na kuomba kuwa akipata nafasi basi atajitahidi kwenda kule kanisani, hasa siku ya Jumapili kama atakuwa amepunguza majukumu.
Dada mtangazaji aliagana na G na kunisimulia kisha tukaendelea na maisha mengine kama kawaida.
Jumapili ilipofika G aliwasiliana na dada mtangazaji ili amuelekeze magali ambapo tulikuwa tunaishi na ndipo hapohapo palipo na lile kanisana.
G alifanikiwa kufika hadi pale nyumbani ambapo tulikuwa tunaishi, mimi dada mtangazaji, mtoto wake na mama yake. Nilifurahi sana kumuona G, nilitamani hata kumkumbatia kwani niliona ni mtu ambaye amekuwa akinipigania sana tangu nilipotelekezwa gesti.
Nilijizuia kumkumbatia lakini furaha isiyo kifani ilionekana katika taswira ya uso wangu. G alikutana na mama akazungumza naye kwani hata yeye elikuwa anahitaji sana kujiridhisha juu yangu.
Basi G alijitahidi kuzungumza na mama kwa kila namna kuhakikisha ana mridhisha mama yule na kweli walikubalina. Baadaye dada mtangazaji akarudi wakasalimiana na G kisha tukaongozana kuelekea kanisani.
Tulimkuta mchungaji na wasaidizi wake wawili, tulikaribisha ofisini, mchungaji alianza kumuhoji G namna ambavyo alikutana na mimi na kwa namna gani nilikuwa nahitaji msaada.
Nilichojifunza G ni mwanaume ambaye hastahili kupewa nafasi ya kuzungumza kwani anajua sana namna ya kupangilia maneno kiasi kwamba ni ngumu sana kukataa au kutokuamini kile anachokueleza.
Nini kilifuatia baada ya G kujieleza mbele ya mchungaji.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U