Saturday, April 8, 2017

Published 4/08/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-46




NILIPOISHIA...

Kwanza yule kaka alianza kwa kunipa pole na ushauri ambao ulianza kunijenga katika fikra zangu, kisha akaniuliza maswali m kadha kwa kadha ikiwemo…

ENDELEA NAYO…

Je, niko tayari kutoka kwenye vyombo vya habari  kama nilivyomwambia awali, nikajibu ndiyo akaniuliza kwa nini ninadhani vyombo vya habari  vitanisaidia, nilimueleza kuwa sina namna kwa sababu nina shida, nahitaji mtoto wangu apate huduma ya kunyooshwa na kupona mguu, sipendi kumuona mtoto wangu akiwa mlemavu.

Na nimekuwa nikiona watu wengi wakisaidiwa kwa njia ya vyombo vya habari basi alikubaliana na mimi , akawaanda wale watu wenye vifaa na kuanza kunifanyia mahojiano kuhusu maisha yangu mwanzo mwisho.

Mwisho aliniuliza swali nimejifunza nini kutokana na tukio hilo? Nilijikuta nikianza kutoa machozi mbele ya kamera na nikamjibu kwa kilio cha kwikwi “wa na u me si yo watu wa zuri, wanapokuwa wanakutaka wako tayari kufanya kitu chochote lakini akishafanikisha basi anakuacha na kukutelekeza, wanawake wenzangi tuwe makini sana na wanaume.” Alimaliza Kecho.
 
Hata yule kaka niliona kama aliguswa na yale maneno  na kilio kile, basi alininyamazisha pale ,muda wote wakati tunafanya mahojiano Gift alikuwa macho na alikuwa akisumbua sana nahisi njaa ilikuwa ikimuuma, nilimwambia yule kaka kuwa tatizo ni njaa akaniuliza kwani nini anampa mtoto ili kutuliza njaa  yake, nilimwambia huwa namnunulia juisi ya embe  ya mia sita kisha nampam kwani sina pesa.

Kweli mule ndani kulikuwa na chupa nyingine ya juisi, na kopo dogo la poda na kimkoba kidogo ndivyo hivyo vilikuwa mezani. Aliagiza juisi nyingine ili nimpe mtoto wangu na kweli aliacha kutusumbua akatulia kisha tukamalizia mahojiano yetu.

Yalikuwa ni mahojiano yenye maswali ya ndani zaidi, sikuwa na aibu ni kama mfupa wa aibu ulikuwa umekatika, nilifunguka kwa sababu nilitaka msaada.

Yule kaka alipomaliza mahojiano akanisaidia pesa kidogo kwa ajili ya kula na alitaka kuhakikisha natoka mule gesti ili kuepusha gharama za chumba.

Je, yule mkaka atampeleka wapi Kecho, wakati yeye anaishi kwenye chumba kimoja na yuko peke yake? Usikose kesho.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
@@@

      edit