Thursday, April 13, 2017

Published 4/13/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA-51







NILIPOISHIA…

G hakuwahi kuja tena pale mgesti ila kila siku asubuhi, mchana na jioni au usiku ilikuwa ni lazima anijulie hali na kunipa mrejesho wa kile alichokifanya juu yangu.
Kuna siku alinipigia simu na kuniambia kuwa amezungumza na ofisa jamii wilaya ya kinondoni ili kuona kama wanaweza kunisaidia.

ENDELEA…
Alinimbia kuwa alifanikiwa kuongea na Ofisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Kinondoni ambaye alisema ni vyema nikaenda kutoa taarifa katika Kituo cha Polisi cha Magomeni kuwa nimetelekezwa na mwanaume gesti na mambo mengine yangefuatia kwa sababu yeye hana mamlaka na jambo hilo kama halijafika polisi.

Hata hivyo yule Ofisa Ustawi alishauri ni vyema pia akatafuta Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Pwani ili apewe taarifa kwa sababu mimi si mkaaji wa wilaya yake ingawa nimepatia tatizo ndani ya wilaya hiyo.
 
G alifanikiwa kuzungumza na Ofisa Ustawi wa Jamii wa Mkoa wa Pwani na akamwambia inabidi niende kwanza kwa mjumbe wa maeneo ninayoishi kwa maana ya kule kijijini, kisha aniandikie barua ya utambulisho, niipeleke ofisi ya serikali ya mtaa naye aidhinishe kama kweli ananifahamu na ndipo niende ofisini kwake alafu atanipelekea kwenye moja ya senta ambayo inatoa huduma kwa watu wenye matatizo kama yangu.
 Nilifikiri nikaona ni mzunguko mkubwa sana alfu sikutaka kurudi tena kule kijijini, nilikuwa kama nimepigwa gazi kwani suala la msaada kwangu lilizidi kuwa gumu.

Wale kina kaka walionirekodi kwenye Global TV Online walikirusha kile kipande kinasambaa na kuenea sehemu mbalimba za duniani. Nilianza kupigiwa simu, kutumiwa sms za pole na za ahadi kuhusu msaada. Kusema ukweli nilipokea SMS na simu nyingi kiasi kwamba nilianza kuchukiwa kwani muda wote simu ilikuwa bize na hata chaji ilikuwa inaisha sana mbaya zaidi nilikuwa napew3a tu pole na kuahidiwa sana, wapo pia waliokuwa wakinitumia pesa kidogo za kula na kujikimu kwa siku hiyo.

Niliendelea na maisha hayo kwa muda, huku nikiendelea kujiuliza nini hatima ya maisha yangu, ndani ya gesti.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
      edit