Nilipoishia…
Basi yule kaka nilimsikia akimshukuru yule mwenye
gesti kwa kukubali kutoa msamaha wa deni la nyumba lakini pia yule kaka
alimwambia yule bosi wa gesti kuwa anikubalie niendelee kuwa pale gesti wakati
anatafuta mahali pa mimi kwenda kuniweka. Yule kaka alikubaliana na mwenye
gesti kuwa zile gharama za malipo atakuwa analipa yeye kwa hiyo nisisumbuliwe
tena.
Endelea…
Sikuwa na amani
nilianza kuona malipo ya ngono nyingine yatatakiwa na yule kaka, akilini mwangu
niliwaza mambo mengi sana, nilifika sehemu nilihisi kutokumwamini sana yule
kaka kwani ni kijana tu, afu anaonekana msela.
Niliendelea kujiuliza sana juu yake. Basi tulirudi wote chumbani kwangu
akanisii mambo mengi sana na kuniambiwa kuwa atawasiliana na wadau wake ili
ajue nini cha kufanya kisha atanijuza.
M&U Foundation ni taasisi ambayo ilianzishwa kwa
mara ya kwanza mwaka 2009 ikiwa ina lengo la kusaidia kutoa elimu ya Afya ya Mama na Mtoto, mwaka
2010 ilibadilishwa na kuanza kutoa elimu ya mtazamo chanya kwa vijana na
ikafanikiwa kuwa inawakutanisha vijana kuanzia sabini hadi mia tatu kila wiki
kwa ajili ya kuzungumza changamoto mbalimba za maisha ya kawaida na mapenzi.
Baadaye
mwazilishi wake ambaye anafahamika kwa jina la Gabriel (Kecho anamuita yule
kaka) alihama mkoa aliokuwa na kwenda mkoa mwingine alipofika kule aliendelea
taasisi ile na kuipa jina ningine la AVIC ambayo ilikuwa inahusika na masuala
ya kilimo cha umwagiliaji kwa sababu mazingira yale aliyohamia yalikuwa ni ya
wakulima.
Mwaka 2013 ilirudi kwenye uhusika wake na kuitwa Mimi
na Uhusiano (M&U) Ambapo mwanzilishi
aliamuwa kujikita zaidi katika kutoa elimu na ushauri wa mahusiano na
ujasiriamali.
Kutokana na simulizi
ya Kecho, Gabriel aliguswa sana na kuona kuwa kuna kila sababu ya kumpigania
na kumsaidia dada Kecho, hakuwa na pesa lakini alijitahidi kwa kila alichokuwa
nacho.
M&U
ilianzisha group mbalimbali za Mtandao wa kijamii wa WhatsApp kwa ajili ya
ushauri basi G aliamua kutumia group hilo kufikisha ujumbe wa Kecho kwa watu ambao
amekuwa akishirikiana nao. Alifikiria sana kitu cha kufanya juu ya Kecho mwisho
akaona ni vyema kama ataadika kitu fulani.
JE,
G anataka kuandika nini kwa ajili ya Kecho na hili group la M&U
litakipokeaje.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U