Nilipogundua kuwa
wanaoweza na mimi tuko sawa kwa kila kitu basi niliamua kujifungia ndani na
kujiuliza, hivi mimi ni nani na nimezaliwa kufanya nini?
Baada ya ‘kujiswalisha’ kwa muda mrefu nikapata wazo la kuanzisha
kampuni yangu ya burudani, nikaanza kujiuliza, je, hiyo kampuni itakuwa inadili
na nini basi nikaorodhesha mambo yote ambayo nayapenda, ikiwemo kuandika,
vitabu, kuwa na vipindi vya redio na runinga, kuwa mshauri au mwezeshaji
(facilitator) na mambo mengine mengi sana.
Nilijiuliza, sheria inanitakaje katika
kuanzisha kampuni hiyo, nikafuatilia, nikajua, nikaandika kila kitu ambacho
kinatakiwa katika kukamilisha kampuni hiyo.
Nikuambie tu katika haya
yote yanahitaji uvumilivu na ufuatiliaji kwani sikufahamu yoye kwa wakati
mmoja.
Baadaye nikaamua kutulia
na kufanya mambo mengine ili nisife njaa ila lengo nagu lilikuwa ni hiyo
kampuni nilichofanya nikawa ni lazima kwa kila siku nijiulize au nifanye kitu
kwa ajili ya kampuni hiyo iwe kwa KUANDIKA, KUTOA PESA, KUELIMIKA, KUFUATILIA
N.K.
Nilifanikiwa kukamilisha
baadhi ya mambo, baadaye nikaisajili ,
nikawa niko nayo kisheria kabisa ila mtaji nikawa sina. Nilichoamua nikaanzisha
shindano la kusaka vipaji vya sanaa.
Nilikuwa na computer moja ambayo ilikuwa mkoa
mwingine basi nikaiagiza, nikaipanga katika orodha ya kuitoa zawadi, nikanunua
na simu ya kunasimu fulani vilitolewa na kampuni ya siku kipindi hicho ilikuwa
inauzwa shilingi 26000.
Nilibakatika kwenda maeneo ya Uganda kwa ajili
ya kufanya mishe fulani ambayo ilibuma nikaamua kununua vitenge, mikoba na vitu
vingine vya biashara, katika mikoba hiyo kulikuwa na mkoba mmoja wa chui chui
niliupenda sana na niliununua bei kubwa kuliko mingine. Nikaona nao niuweke
kwenye zawadi kwa upande wa wanawake.
Basi nikafanya matangazo,
nikiwa nimemuazima na kusaidia na mama yangu pesa zingine. Nilijitahidi sana
kufanya matangazo kwa kuwashirikisha wadau mbalimbali, hatimaye siku ya tukio
ikafika. Nikawa nimemuagiza mtu wa mapambokwenda kupamba eneo na jukwaa,
alipenda akakuta watu wengine nao wanapamba ndani ya ukumbi mmoja.
Nini kiliendelea, usikose kufuatilia mada na
simulizi hii ambayo itakufanya kuondoa katika kutafuta mafanikio.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U