NILIPOISHIA…
Tulipofika
kituoni G aliomba kutupiga picha ya kumbukumbu tukiwa kituoni hapo, mimi, dada
mtangazaji na mkaka mmoja ambaye alikuwa anatangaza na dada yule.
ENDELEA…
G alitupiga
picha na kutuaga tukaingia kwenye daladala na kuelekea Kimara nyumbani kwake na dada mtangazaji, ambaye
alikuwa anaishi, yeye, mama na mtoto wake.
Nilichojifunza
kwa G kila hatua niliyokuwa nikienda alikuwa ananieleza kuwa ninakoenda kuishi
si kwetu, naenda kuishi na ndugu baki inawezekana nikawa nanyanyaswa, natukwana
na mambo mengine kadha wa kadha lakini, nijaribu kumsoma mtu ninaye ishi naye
na niweze kuishi naye kwa jinsi yeye anavyotaka.
Nilimsikiliza na kumuahidia kuwa nitakuwa
mvumilivu katika kila hatua na kama kuna jambo ambalo litakuwa linanisumbua
basi nitamshirikisha mapema. Kwani G aliamua kujitoa na kunisaidia kwa moyo
mmoja bila kudai malipo yoyote yale,. Nilimuheshimu na kumpenda sana G kila
jambo nililokutana nalo nilikuwa namshirikisha.
Kitu
nilichoshukuru nhata dada mtangazaji hakuwa na roho mbaya kwani alinipokea
vyema na kuniambia kuwa kitu kitakachopatikana tutakuloa wote kikikosekana basi
tuna shukuru Mungu lakini pia akanigusia kuwa niwe makini na mama yake kwani
anaumwa kuna wakati alikuwa kama amepooza, afu ni mtu mzima kwahiyo kama kuna
mambo ambayo nitakuwa sijayaoenda basi nimuelewe mama yake ni mtu wa aina gani
na niwe na mwambia yeye.
Mama yake
mtangazaji alinipokea na akaniuliza maswakli kadhaa nikamjibu lakini
alichomwambia dada mtangazaji, ajitahidi awasiliane na G ili aje akazungumze
naye, hata kama kuna jambo linatokea kwangu wawe wanafahamu ni wapi kwa
kuanzia.
Nili kilifuatia baada ya mama
mtangazaji kusema vile?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba,
Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na
M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U