Napenda kukukalimisha
kwenye mada yetu ya ujasiriamali. Umeshawahi kujiuliza kwa nini ngumu kwa wewe
kutimiza ndoto zako? Leo kwenye tutazungumzia ni kwa nini ndoto yako isitimie
wakati ukiwa hai, najua kuna changamoto na magumu mengi sana ambayo unakutana
nayo katika maisha yako.
Lakini kaa chini na
ujiulize kama usipotimiza ndoto yako nani atakuja kukutimizia na kama watu wote
wasingetimiza wajibu wao wa kutimiza ndoto zao dunia ingekuwa wapi leo,
changamoto na matatizo yaliyomo duniani nani angepata mbadala wake.
Hivi kuna sababu gani
zinakufanya usitimize ndoto au malengo yako , kama ni muda kwa nini usiwaze
namna ya kukabiliana na hiyo changamoto inaumiza sana kumuona mtu mwenye ndoto
nzuri na za maana zinaishia kuajiliwa au kusikojulikana.
Unapaswa ujue vitu ambavyo
vinasababisha ndoto yako isitimie ili kila kukicha uwe unapambana navyo kuepuka
visiwe kikwazo cha wewe kutokutimiza ndoto zako.
Hakuna ndoto ambayo
inaweza kutimia bila kuumia au kutumia muda na rasilimali watu, muda na
kadhalika.Inauma sana ninapoona vijana wengi wa kike wakishindwa kutimiza ndoto
zao kwa sababu tu wameolewa, walipigwa mimba, walitelekezwa, walifiwa na wazazi
au walezi wao, eti kwa sababu tu alifeli mtihani wake wa mwisho na wengine
wakihisi hawawezi kutimiza ndoto zao kwa sababu tu waliwahi kubakwa na jamaa
yake wa karibu au watu asiyowafahamu.
Acha kukumbuka matatizo
yako bali tafuta nja mbadala wa kujikwamua na umaskini ili uifikie ndoto yako.
Usikose kesho kwenye muendelezo wa mada hii.
Tukutane kesho kwenye mada nyingine
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba,
Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na
M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U