Nimshukuru Mungu kwa
kuimaliza siku salama, lakini nimejifunza kitu kikubwa sana baada ya kwenda
kumtembea jamaa ambaye alipata ajali ya kusababishiwa na kutoboka jicho moja na
jingine kupofuka sambamba na kupooza kwa mikono yake, huku mkono mmoja
ukihitaji kufanyia upasuaji lakini kwa kuwa pesa hana imemladhimu kukaa tu
ndani.
Nilichofarijika zaidi na
nilichojifunza UPENDO WA DHATI HUWA HAUISHI kwani pamoja na magumu aliyonayo
jamaa huyo lakini mkewe ambaye tena hawakufunga ndoa ameendelea kuwa na mpenzi
wake pasipo kumkimbia, anampenda na yuko naye bega kwa bega, hivi wewe kwa
mbwembwe zako unaweza kweli kuvumilia magumu hayo kama hauwezi kwa nini UNATAKA
MPENZI MWENYE UPENDO WA KWELI!?
Wewe na mimi si wema wala
wazuri na watakatifu sana mbele ya Mungu lakini kwa upendo wake ametuacha tuwe
salama kama tulivyozaliwa. NI FUNZO NA SOMO KUBWA SANA KWETU.
WIKI iliyopita
nilizungumzia namna ambavyo mtu akiwa na dhamila ya kweli ya kutoka moyoni basi
ana nafasi kubwa sana ya kuweza kufikia malengo yake aliyonayo. Kama alipanga
kuwa Kiongozi mkubwa serikalini, shuleni, kazini, kuwa mwasayansi, daktari, mtu
maarufu, muigizaji, muimbaji, mwandishi, mkulima, muuza mkaa, machinga, mchimba
mitaro, mvuvi, Staa na vinginevyo. Inawezekana kama ukiwa na nia pia ukawa na
malengo.
Nilisema pia dhamila hiyo
inaweza kuwa kubwa au ndogo kwa mfano mtu anataka kufungua shule au hospitali
yake anaweza kufikia malengo hata kama atakuwa hana kitu lakini kama ana
dhamila na malengo basi ipo siku atafikia pasipo kujali umbali na magumu
atakayokutana nayo.
Usikose kesho…
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
@@@@