NILIPOISHIA…
Yule kaka alipomaliza mahojiano akanisaidia pesa
kidogo kwa ajili ya kula na alitaka kuhakikisha natoka mule gesti ili kuepusha
gharama za chumba.
TIRIRIKA….
Kaka alionekana kuwaza sana juu ya sehemu ya
kunipeleka, nilimwambia kuwa natamani hata anitafutie kituo chochote cha watoto
yatima ili nikamuhifadhi mwanangu kisha niingie mtaani nitafute kazi na
nitakuwa naenda kumsalimia mwanangu Gift.
Kaka aliendelea kuwaza na kuwazua, mwisho aliomba
kuonana na mmiliki kwa gesti ile ambaye alikuwa ni kijana tu. Mwenye gesti
alifika akazungumza naye na kumwambia kuwa hata yeye hakuwa na pesa za kulipia
gharama zile za chumba kwa muda ule kutokana na kupanda zaidi lakini yule kaka
alitumia maneno ya hekima na busara kuzungumza na kushauriana na mwenye gesti.
Mwisho
walikubalina na mwenye gesti kuwa lile deni la awali lote na yeye ananisamehe
kama mwanadamu ambaye nimekumbwa na matatizo ila aliomba nimwachie chumba chake
ili aendelee kufanya biashara.
Walizungumza sana na yule kaka, swali lao kubwa
lilikuwa ni wapoi nitaenda maana kule
Kwa Mfipa nisingeweze kwenda tena na wala kule kijiji kwa mama sitaki
kukanyaga.
Na hata kama
nikikanyaga kule sitakuwa na msaada wa kuweza kumtibu mwanangu, ni heri
niendelee kupigana mjini hivyo hivyo ili mradi mtoto wangu anyooshwe mguu.
Ninaweza kurudi kijijini lakini muda wa kuhudhuria klink ukifika nitapata wapi
pesa ya kwenda na kurudi mara kwa mara, nitapata wapi gharama za matibabu na
mahitaji ya mtoto kama kula, kunywa na vitu vingine.
Basi yule kaka nilimsikia akimshukuru yule mwenye
gesti kwa kukubali kutoa msamaha wa deni la nyumba lakini pia yule kaka
alimwambia yule bosi wa gesti kuwa anikubalie niendelee kuwa pale gesti wakati
anatafuta mahali pa mimi kwenda kuniweka. Yule kaka alikubaliana na mwenye
gesti kuwa zile gharama za malipo atakuwa analipa yeye kwa hiyo nisisumbuliwe
tena.
Je, nini kiligonga kichwani mwa Kecho baada ya
mtu anayemsidia kuomba andelee kuwa pale gesti na yeye ndiye atakayekuwa
analipia?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba,
Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na
M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U
@@@