Kila kitu huwa ni malengo
na dhamila ya ndani ambayo inaweza kukufanya ukafikia malengo.
Bila kujali ni umbali gani
wa kuyafikia malengo husika lakini kikubwa ni kuyafikia.
Napenda kushirikiana na
wewe mwanaM&U kuwa kama una nia na jambo fulani amini kuwa unaweza
kulifikia Kwa KUDHAMILIA. MALENGO, KUJITUMA NA HESHIMA kila jambo linahitaji
vitu hivyo.
1-DHAMILA
Ni msukumo wa ndani ambao
unakusukuma na kukukumbusha kuwa mbona hujafikia lengo lako la kuwa msanii mkubwa
wa muziki, filamu, kuchora, kuwa mfanyabiashara mkubwa, msusi maarufu, mwalimu
mzuri, Daktari bingwa. Mwanamasumbwi na kadhalika.
dhamila inakukumbusha hata
pindi unapokuwa umekata tamaa umechoka kabisa ila unasikia sauti kutoka ndano
yako ikikuambia kuwa"hivi.unajijua kuwa wewe ni mwanajeshi, msomi wa chuo
kikuu, mbona una kata tamaa wakati umebakisa sehemu ndogo tu kufikia malengo
yako, nyanyuka bhana aja uvivu pigana, usidhani Mo, Bakharesa, Dk. Mengi,
Shigongo, Ben Po, Maua Sama, Ay, Diamond, Jide, Madam Ritha, Angelina Jolie,
yvone Chaka Chaka, Zitto Kabwe, Mwigulu Nchemba, Tundu Lisu, Halima Mdee na
wengineo.
Walifika hivi hivi hapo
walipo, la hasha wamelala sana njaa, wametembea sana wakiuza vitumbua, wamelima
sana vibarua na wameteseka sana lakini unaona leo wanakula bata. Sasa nawewe
amka ndugu yangu pigana, usikubali kushindwa, ebu tafauta wimbo wa
Kimbia-Kidumu-Songa Mbele-Alfa, Jikubali-Ben Pol, Don't stop until u get enough
- Michael Jackson na nyingine nyingi zenye kukuhamasisha na kukupa hali
mpya."
Sauti ya dhamila ni yenye
matumaini, upole, ukarimu, ujasiri na uthubutu ndani yake, isikilize na ifanyie
kazi huweza kufilia malengo bila kukutana na changamoto, utahadithia nini
kuhusu mafanikio kama unataka kuyapata bila kuyahangaikia.
Kila mtu ana matatizo yake
wakato mwingine ya kwako ni madogo sana kuliko ya mwenzako, jaribu kujifunza
kwa watu wenye ulemavu ambao walijikubali na hatimaye wakatumia karama zao na
mwisho wamefanikiwa kisha nifananishe na wewe ambaye umekamilika kabisa. Je,
yule mlemavu mwenye mafanikio angekuwa kama wewe angekuwa wapi na wewe kwa
uvivu wako na ujinga ulionao ungekuwa kama yeye ungelikuwa wapi? Ninaamini ungekuwa ni mtu wa kuombaomba kisa
huu mlemavu. Achana na dhana potofu kuwa huwezi kutajirika kwa sababu hauna
kile na hiki.
Usikose sehemu inayofuatia
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba,
Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na
M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0679979785.Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U