NILIPOISHIA…
Kusema ukweli
nilipokea SMS na simu nyingi kiasi kwamba nilianza kuchukiwa kwani muda wote
simu ilikuwa bize na hata chaji ilikuwa inaisha sana mbaya zaidi nilikuwa napewa
tu pole na kuahidiwa sana, wapo pia waliokuwa wakinitumia pesa kidogo za kula
na kujikimu kwa siku hiyo.
ENDELEA NAMI…
Kweli kwenye
mamba na kenge wamo, kwani wapo wanaume ambao walitumia nafasi hiyo ya matatizo
yangu kunishawishi kutembea nao.
Wanaume wakware hawakuacha kunisumbua kiwa
kuniahidi kuwa wanitumie nauli niwafuate mahali walipokuwa lakini nilikuwa
nishang’atwa na nyoka kwa hiyo hata jani tu liliponigusa nilishituka sana.
Nilipata shida
sana kwani wanaume wengi walipata nafasi ya kutaka kutumia tatizo langu ili kufanya mapenzi na
mimi, nashukuru Bro G alinieleza na kunishauri mambo mengi sanaa kuwa kuna watu
watajitokeza kunisaidia ila kwa nia ya kufanya nao mapenzi, hivyo nilikuwa na
tahadhari sana kwa kila anayepiga simu.
G na wanachama wa M&U waliendelea kunisaidia kwa kunilipia pale gesti, siku zilienda msaada ukiwa bado haujapatikana, kaka G aliendelea kuumiza kichwa ni kwa namna gani atanitoa pale gesti? Na atanipelea wapi.
Baada ya
kuumiza sana kichwa, Bro G akapata jibu la kuzungumza na mdada mmoja
ambaye ni mtangazaji wa redio moja
jijini Dar.
G alitumia
nguvu nyingi sana kumshawishi mdada huyo mtangazaji, na kumuaminisha kuwa mimi
ni mtu mzuri na nina hitaji msaada wake na wao.
Hatimaye yule
dada alimkubalia G ila kwa masharti kuwa kila siku awe anapata taarifa zangu ,
asije kuwa amenitelekeza kwa huyo dada.
G alikubali na
kumuahidi yule dada kuwa watakuwa bega kwa bega hadi mwisho wa suala langu.
Dada mtangazaji alikubaliana na G na kumuahidi anipeleke siku inayofuatia.
Mpenzi msomaji,
ilikuaje, baada ya Kecho kupata mtu wa kumsaidia kuishi naye kwa muda?
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwa ku-Bonyeza Hapa
Na.M&U