NIMSHUKURU
Mungu muumba wa mbingu na aridhi kwa kunipa pumzi ya kuweza kujadiliana nawe
leo.
Mada ya
leo itahusu aina ya hulka (tabia za asili) za watu ambazo zinawaongoza katika
kufikia mafanikio yoyote yale.
Tabia
hizo zimewafanya watu wagawanyike katika makundi ya aina tatu ambayo ni:
WASIOWEZA KUFANYA KITU
Yaani
mtu wa kundi hili anahisi yeye amezaliwa kuwepo tu duniani na kuangalia namna
ambavyo dunia inaenda au kuendeshwa na wengine. Katika fikra za mtu wa kundi
hili la kwanza yeye hujiona kuwa ni watu wanyonge, dhaifu ambao hawawezi
kufanya kitu chochote katika dunia hii, yaani hata hawana hata muda wa
kuifikirisha akili zao, hata kwa jambo dogo tu la kutengeneza jembe
linapoharibika hawawezi kufanya kitu hicho.
Mara
nyingi watu wa aina hii wao hutegemea au husubiri mtu mwingine afanye ili wao
wapate au wapokee. Je, na wewe uko kundi hili?
WASIOKUBALI MATOKEO
Mara
ngapi umeshuhudia kukataliwa kwa jambo f’lani ambalo limefanyika ndani ya
familia, kijiji, darasa au eneo unaloishi? Lakini eti kutokana na ukubwa wa
jambo lenyewe kila mtu anakataa kuwa aliyelifanya sio yeye. Sasa kama sio yeye
ebu kamlete huyo unayedhani kalifanya. Hawa ni baadhi ya watu wa kundi la pili
ambao katika akili zao hawaamini kama f’lani anaweza kufanya jambo.
Naamini
kauli za kumbeza mtu aliyefanya kitu f’lani umewahi kuzisikia sana.
Acha
kuiishi kwa mazoea eti kwa kuwa wewe ni mlemavu, sio msomi, msomi, maskini, wa
kijijini basi huwezi kufanya kitu, hapana si kweli! Kemea fikra hizo ni fikra
za kimasikini nani kakwambia kuwa na maendeleo kuna hitaji wewe uwe na hicho
unachofikiria kinakukwamisha.
Amini
nakwambia ndani yako kuna kitu Mwenyezi Mungu kakiweka labda hujakifahamu au
hujajua namna ya kukitumia.
Kama
ilivyo mistari ya kiganja chako haifanani na ya baba, mama, mkeo au mtoto wako
na ndiyo akili za mwanadamu zilivyo. Je, uko kundi hili?
WAPO TAYARI KUTHUBUTU
Kundi la
mwisho ni lile la watu mwenye kuthubutu, kutenda, akili zao hazikubali
kushindwa wanaamini kabisa wameletwa duniani kukifanya hivyo wanajitahidi
kufanya kila namna ya njia ilimradi waweze kutimiza na kuishi katika ndoto zao.
Ndiyo
maana muda huu unasoma makala hii kwa sababu ya mwanzilishi na mbunifu wa
mtandao wa WhatsApp ambaye amekuwezesha wewe kupata makala haya kwa wepesi na
rahisi zaidi.
Muda huu
unaperuzi simu yako kwa sababu tu ya mtu mmoja aliyekuwa anaitwa Steve Job (kwa
sasa ni marehemu) alithubutu kufikiria na kugundua simu ya smartphone kama
ambavyo unaskroo chini kusoma mada hii ya ujasiriamali.
Hivi
kweli akili yako unataka kuniambia ni nyeupe, pee! Kwamba haina kitu ambacho
inaweza kukifanya chini ya jua, hapana si kweli na hata kama umekuwa ukiwaza
hivyo kuwa wewe huwezi kufanya kitu unakuwa unakosea sana. Amka ndugu yangu,
fikiria, pata muda wa kukaa sehemu tulivu na fikiria nini unaweza kukifanya
bila kujali mapungufu au madhaifu uliyonayo au yanayokuzunguka.
MUNGU AKUBARIKI KWA SOMO HILI.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U