Tuesday, January 17, 2017

Published 1/17/2017 06:00:00 PM by

HUJAJUA TU KWA NINI ULIACHWA NA MPENZI WAKO!



Mpenzi msomaji nikukaribishe katika siku nyingine katika kujadiri mada za mahaba. Leo nitazungumzia wale ambao wameachwa na wapenzi wao lakini mpaka kesho kutwa hawajajua ni kwa nini wameachwa!


Kimsingi kila kitu ili uweze kukifanya kwa uhakika ni  vizuri sana kukifanya huku ukiwa unakifahamu kwa undani hii itasaidia wewe kujua kile ulichokuwa unakifanya na unachokifanya. Kama ni biashara basi isome kwa kujifunza sio mpaka uende darasani, kama ni mpenzi ni vizuri sana ukapata muda wa kumsome mpenzi wako ili hata kama utaingia kwenye uhusiano utakuwa unamfahamu A-Z.

Wapenzi wengi wamekuwa wakipata wakati mgumu sana pindi wanapoachwa na wapenzi wao baadhi wamejikuta wakiangukia kwa wapenzi wapya ambao pengine walikuwa hawawapendi au hawakuwahi kuhisi kama watajihusisha nao katika suala zima la uhusiano. 
 
Wakati huo kuna wengine wamejikuta wakiingia kwenye uhusiano mpya na kufurahia penzi jipya kwa kumpata mtu sahihi ambaye kimsingi amerudisha huzuni yake iliyopote  kwa muda mrefu lakini pia wapo wengine ambao wameangukia za uso kwa sababu tu hawakupata muda wa kujiuliza ni sababu zipi zilichangia wao kuachwa au kuachika. Kwa kufanya hivyo amejikuta akikurupuka na kujiingiza kwenye uhusiano na mtu ambaye si sahihi.

Muungwana anapokosea kitu hata kama alibisha kwa kiburi cha kibinadamu , pesa, elimu, ubavu na mengineyo ila akipata muda wa kutafakari mambo yote aliyoyafanya siku nzima, anajitahidi kujiuliza Je, nini chanzo ya kile kilichotokea? Je, yeye ndiye mwenye makosa au aliyemuacha? Na kama ndiye amejipangaje kuanzisha uhusiano mpya kwa kukwepa sababu au chanzo cha yeye kuachwa?

Kwa mfano kama mwanaume ni mlevi kupindukia basi anajitahidi kupunguza au kuacha kabisa kama ni mwanmake ambaye alikuwa kila kukicha ni kiguu na njia basi anapunguza au kuacha kabisa na anafanya hivyo ili aende sawana mpenzi wake.

Jifunze kujifanyia tathimini kwa kila jambo iwe maisha ya mapenzi kwa maana ya kukubali kama umekosea lakini pia maisha ya kibiashara kukubali pindi unapopata hasara ili kuweza kujua ni namna gani awamu ijayo haupati hasara.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U

      edit