Karibu mpenzi kwenye mada ya leo ya UJASIRIAMALI
ambayo inazungumzia kuhusu tabia ya kujenga ujasiri ili kukufanya usimame tena
katika maisha yako.
Hii ni sehemu ya mada ambayo ilijadiliwa jana
kwenye Semina ya Mimi na Uhusiano (M&U) iliyofanyika majuma kadhaa yaliyopita. Shukrani za
dhati ziwaendee wale wote walioweza kufanikisha kwa namna yoyote ile kukamilika
kwa semina ile, wawezeshaji waliohudhuriana na kadhalika.
Maisha ni mapambano kwa mwanajeshi aliyekomaa
anayekuwa yuko vitani au mwenye hali ya kutaka kushinda vita huwa hakimbii vita
bali hukabiliana nayo na hata kama akipigwa hakimbii vita bali hukimbia sehemu
na kujificha ili kujipanga na kubadilisha mbinu za kukabiliana na adui wake.
Kama wewe ni miongoni mwa watu ambao wamekata
tamaa na maisha au biashara kutokana na kufanya kazi au biashara fulani kwa
muda mrefu lakini huoni mafanikio yake, umekuwa ni mtu wa hasara, usilalamike,
najua unaumia lakini umia kwa muda kisha jipange upya, jenga usajiri mwingine
utakaokufanya usimame upya kwa kutumia njia nyingine.
FANYA HIVI
Orodhesha madhaifu na magumu yako yote ambayo
umekuwa ukikabiliana nayo au magumu yote ambayo yanakutatiza katika kutimiza au
kufikia malengo yako kisha jiulize ni kwa nini ushindwe kutoboa kwa sababu ya
ugumu huo, je ni nini kinachangia uwepo wa ugumu huo. Ni vitu gani vitakufanya
uweze kuutatua ugumu unaokukabili.
JIFUNZE KWA WALIOTANGULIA
Ukiweza kujua hayo fanya kila njia ili kusoma
au kujifunza namna ya kukabiliana au kupigana na ugumu unaokusumbua kwa
kujifunza kutoka kwa watu ambao wamefanikiwa kwa kuangalia mazuri yao ambayo
wameyafanya kwa kuwasoma, kuzungumza nao na kadhalika.
LAZIMA UWE NA MTAZAMO CHANYA
Hakikisha akili yako imeishajianda kwa ajili
ya mabadiliko yako kwa kila namna ili mradi uwe mwenye mtazamo chanja wenye
mafanikio mema.
Kwani kujituma bila kuwa n a mabadiliko ni
sawa na kazi bure, utajikuta unafanya kitu lakini hauna mabadiliko yoyote
kwenye akili yako
UDHAIFU USIUPE NAFASI
Achana natabia ya kuendelea kufikiria kuhusu
madhaifu ambayo umekuwa ukikutana nayo, acha kufikiria kuhusu ni namna gani
ulifeli bali fikiria ni kwa njia zipi hutafeli tena kwa awamu nyingine,
ukiendelea kufikirianamna ulivyofeli utashindwa kusonga mbele na kujiona ni
mnyonge mtu usiyestahili kufika unakotaka kufika wakati ukweli ni kwamba lazima
changamoto ziwezo ili uweze kufika unakostahili kufika.
KARIBUNI KWA MAJADILIANAO KUHUSU MADA HII YA
UJASIRIALIMA.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U