NAPENDA Kumshukuru Mungu
kwa kila jambo katika maisha yangu ya kila siku, kwani ni kwa rehema zake tu
ndizo zinanifanya nakutana nawe msomaji wangu.
Leo nitazungumzia jambo
ambalo wapenzi wengi wamekuwa wakilichukulia mzaha na kuliona la kawaida lakini
kiukweli ni lakukemea sana, hivi inawezekanaje mkashea penzi na vitu vingine
lakini kwenye kuchangia simu iwe tatizo!
Binafsi naona hapo kuna
tatizo kubwa sana, tatizo ambalo ukijiuliza mara mbili mbili utagundu
linaongozwa na usaliti wa chini chini wa wapenzi husika. Siku zote imezoeleka kuwa
mwanamke na mwanaume wanapoamua kuishi pamoja ni kama wameungana na kuwa kitu
kimoja, ndiyo maana shuka yao ni moja. Wanakula chakula pamoja, wanafanya mambo
mengi pamoja lakini kwa nini kwenye kushea simu kuwe na tatizo, usiri huo ni wa
nini? Na kwa nini? Kama sio kudhihirisha kuwa wewe ni mchepukaji na kwenye simu
yako kumejaa madudu yako kisa mwenzio hashiki simu yako, ni nini?.
Ni dhahiri kabisa kuwa
kizazi hiki kimetawaliwa na jinamizi wa uasherati, haiwezekani simu ya mwenza
wako iwe siri kiasi hicho, la hasha! pana jambo ndani limejificha.
Hilo ni janga,
inasikitisha, haileti mantiki kwa wapenzi wawili wenye mapenzi ya dhati,
uaminifu na wanataka kujenga familia bora kufichana kilichomo ndani ya simu.
Nini kinakufanya mpenzi
wako, mumeo, mkeo asishike simu yako, tena ukiona anaelekea kwenye kugusa
sehemu ya picha (gallery) mamaaa...! ndiyo unampokonya kabisa mkeo simu yako na
kumtupia maneno makali; “Nani kakuambia ushike simu yangu, unatafuta nini huko.
Kila mtu ashike simu yake, mambo yakusachi vitu vyangu sitaki.’’ Hapo kama mwanaume hataki mkewe ashike simu
na mwanamke hataki mumewe au mpenzi wake aguse simu yake unategemea nini?
Si inaonyesha kabisa kuwa kizazi hiki
cha ‘dot com’ kimejaa usaliti. Ukiona mpenzi wako hataki kushika simu yake basi
ujue hilo ni jipu tena jipu uchungu ambalo halihitaji hata kusubiri liive ili
litumbuliwe, wewe libonyezebonyeze tu utaujua ukweli.
Kwa ushauri na maoni tembelea ukurasa wetu wa Mimi na
Uhusiano kwenye Mtandao wa Kijamii wa Facebook, Ista:mimi_na_uhusiano au jiunge
kwenye group letu la WhtsApp kwa namba iliyopo juu.
Itaendelea...
Usikose sehemu ya pili ya mada hii.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U