NILIPOISHIA…
Ni mwanaume gani wa miaka zaidi ya
ishirini na tano unashindwa kujitegemea!? Unashindwa kuwa na maamuzi yako
binafsi kuhusu maisha yako!? Unakuwa mwoga na maisha, kama mwanaume unakuwa
mwoga kiasi hicho vipi kuhusu dada zako!? Hii ni hatari na madhaifu makubwa
sana kwa Maiko.
ENDELEA…
“Mungu mbona natesekana hivi nini kosa
langu, nilijikuta naanza kulia nikiwa usingizini huku nikiwaza. Ghafla
nikashtushwa na sauti ya kondakta akiomba hela ya nauli. Nilijifuta machozi ya
uchungu kwa kutumia blauzi yangu niliyokuwa nimeivaa kisha nikafungua kifungo
cha kwenye kanga yangu na kutoa shilingi elfu saba niliyokuwa nayo na kumlipa
konda.
Nilimtazama mwanangu kwa jicho la huruma,
maskini Gift mwanangu wala hafahamu yanayomsibu mama yake, nateseka mwanangu
Gift, ukikua usome sana kwa bidii, sawa
mama, kwa mateso haya ninayoyapata natamani ningekuwa mtoto kama wewe, pengine
ningetamani niwe mtoto siku zote kuliko mateso ninayoyapata.
Hatimaye konda alitangaza kuwa tumefika
Kibaha Kwa Mfipa mkoani Pwani. Nikashuka na kuelekea moja kwa moja kwa rafiki
yangu wa siku nyingi maarufu kwa jina la
Minza, ni mdada maybe alikuwa amepanga kichumba kimoja hapo Kwa Mfipa.
Minza aliponiona kwa jinsi nilivyokonda na
kuchoka alinishangaa sana, pamoja na kuwa mimi ni mwembamba lakini kwa mshangao
wa rafiki yangu Minza nilibaini kuwa nilikuwa nimekonda vibaya sana.
“Eeeeh! Na wewe mbona umekonda hivyo,
umepaukawee, umekuwa mbaaaaya, ndiyo kusema maisha yamekushinda huko kwa mumeo
au?”
“Ni heri yangekuwa yamenishinda
mwenzangu.”
“Ila, umefumaniwa.”
“Ingekuwa angalau!”
“Kulikoni Kecho, nini sasa?”
“Shosti kama una chakula, chai, uji au
chochote cha kula naomba japo nipoze njaa, maana toka asubuhi sijatia kitu
mdomoni mwangu. Hapa unavyoona mwanangu Gift
hajanyonya muda mrefu kwa sababu maziwa yangu ni kama yamekauka kwa
sababu ya njaa, mateso na mawazo ya muda mrefu.
Gift wangu. Maskini kalia weeeee hadi
akapitiwa usingizi. Mimi shosi nipo
nitakupa mchapo mzima wala usjili.”
Nashukuru Minza kwa uji, kidogo angalau
naweza hata kuongea, mwanzoni nilikuwa naona kama na wewe unaning’onga tu, mimi
na njaa na uchovu afu wewe unataka umbeya tu.
Kwanza shoga yangu naomba nipumzike hapa
kwako kwa siku kadhaa wakati najipanga kwenda kijijini kwetu, si unajua palivyombali
na hata mia yenyewe sina
Je,
Minza alimkubalia rafiki yake, usikose kesho muda kama huu.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na:M&U