NILIPOISHIA…
Niliendelea kupiga kelele za uchungu ,
huku nikimuita mama yangu, mamaa mamaa, nahisi mtoto anashuka mama, mama
nisaidie, mama.
SONGA NAMI…
Niliendelea na hali ile kutokana na
maumivu ambayo nilikuwa nayasikia. Mama alihisi kitu akanipeleka kwenye kichaka
kidogo ili hata kama kuna mtu anapita asiweze kutuona kisha akatandika kitenge
chake alichokuwa nacho nakunikalisha, kwa kuwa tumbo nilikuwa nsikia uchungu
mkubwa nikajikuna nimekijla huku mwili wangu ukilazimisha kusukuma mtoto.
Niliendelea kusukuma mtoto huku nikiwa
nimeyang’ata meno yangu kutokana na uchungu niliokuwa nausikia huku machozi
yakinitoka kwa mbali.
Mama naye nikimuona akihaha huku na kule
mara anakimbia kwenye kinjia ili kuona kama atapata msaada wowote wa kuweza
kuniwashisha zahanati lakini wapi.
Mama anarudi tena kuja kuniangalia na
kunihimiza sukuma mwanangu, jitahidi tu mama,
nikazidi kusukuma, ama kweli mwanamke kweli anazaa kwa uchungu,
nikiendelea kusukuma kwa uchungu sana, huku machozi yakinibubujika.
Hali ile iliendelea mara kwa mara kwa mama
yangu, kiukweli nilimuona mama kama namtesa sana, raha zangu na Maiko lakini zinamsumbua mama, niliumia
sana, na ndipo nikatamani kukitoa kiumbe kile tumboni mwangu kwa jazba,
nikasukuma kwa nguvu.
Nikamuona mama akisongelea eneo langu la
mapajani na kunyoosha mikoni yake kama anapokea kitu, huku akiendelea
kunisisitiza kusukuma, nilisukuma kwa nguvu hatimaye mtoto akatoka, na mama
akazidi kumvuta mtoto.
Nini
kilifuata baada ya Kecho kujifungua akiwa polini, je, wataendelea na safari ya
kwenda zahanati au watarudi nyumbani.
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au
tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U