Wapenzi msomaji karibu
sana kwenye mada ya ujasiriaali ambapo leo ninazungumzia biashara ya chakula na
umuhimu wake.
Ukiangalia moja ya
mahitaji muhimu katika maisha ya mwanadamu ni chakula, kwasababu ili uwe na
afya bora ni lazima ule chakula, tena sio chaula tu bali chakula bora chenye
virutubisho vyote. Ili uweze kufanya kazi ni lazima uwe umeshiba vizuri.
Kwa maana nyingine
biashara ya huduma ya chakula ni nzuri sana kwa mtu anayehitaji kuifanya lakini
kabla ya kuamua kufanya biashara hii lazima uzingatiwe mambo yafuatayo;
Sehemu yenye umati wa watu
Ili kufanya biashara yako
kuwa ni nzuri tafuta sehemu yenye umati wa watu wengi, kwa mfano kwenye
viwanda, gereji, mashineni, shuleni na kwingineko, maeneo haya yanakuwa na
umati mkubwa wa watu, kwa hiyo utakuwa na uhakika wakuuza chakula chako vizuri.
Aina ya vyakula
Ukishaanza biashara ya chakula
baada ya muda utafahamu chakula gani na muda upi wateja wako wanahitaji chakula
.
Kama ni asubuhi tengeneza
chai, chapati, maandazi, maharage, hata na supu, mchana ugali, wali, pilau na
mboga za majani na zinginezo.
Bei ya chakula
Ni lazima ujue kwa eneo
ulilopo na huduma ya chakula unayotoa, unaopaswa uuze chakula chako kwa bei ipi
ambayo wateja wako watakuwa tayari kulipa bila matatizo.
Andaa chakula kizuri
Kila kitu kinatakiwa
maandalizi mazuri, tafadhali fanya utaratibu wa kuandaa chakula chako mapema
ili kiwe bora na chenye kuvutia kwa wateja wako.
Zingatia usafi
Suala la usafi ni jambo muhimu
sana katika maeneo ya biashara hasa biashara ya chakula na vinywaji, mara
nyingi wateja wanaokuja ni wa aina mbalimbali kwahiyo wako ambao usafi kwao ni
kipaumbele na kama ikibainika wewe huna sifa ya usafi unaweza kujikuta
ukipoteza wateja wengi zaidi kwa tabia hiyo.
Kauli nzuri
Upole, ucheshi na ukarimu
ndizo lugha za biashara siku zote, lakini wafanyabiashara wengi hujisahau hasa
baada ya kuona ameanza kupata mafanikio na wateja wa kutosha na kusahau kuwa
lugha nzuri iliwavuta na matokeoa yake anaanza kutoa lugha za maneno ya ukali
na dharau kwa wateja wake, cha kujifunza biashara haihitaji mazoea.
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali.
Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745 au 0679979785.
Na.M&U