WASOMAJI wa ujasiliama leo
tunakutana tena kama kawaida katika kuzungumza namna ya kujikwamua katika ugumu
wa maisha tulio nao na kuwa kwenye mafanikio.
Wiki iliyopita tulijifunza
kuwa na kipaumbele katika kazia, shughuli au maono yetu,lakini vyote hivyo
haviwezi kwenda bila kujituma na ndiyo maana mada ya leo nitajifunza nanyi
zaidi juu ya kujituma na faida yake.
Siri na mbinu kubwa ya
kufanikiwa ni mtu kujituma, kufanya kazi kwa bidii, kama kweli ukitaka uwa
mjasiriamli mwenye mafanikio katika
shughuli zako ni lazima ujitume kweli,
achana na tabia ya kusukubwa sukumwa, kuambiwa ambiwa hata kama haujaajiliwa
jenga utaratibu wa kufanya kazi kwa bidii na mwisho wa siku utaona mafanikio
yake.
Mfano mzuri, kuna baadhi
ya nchi duniani kama india, Indonesia na zinginezo zilikuwa na uchumi mdogo
sana lakini mwisho wa siku waligundua tatizo lao na kuligeuza kuwa mafanikio
kwa jituma katika kazi zao na leo hii unavyosoma makala hii, india inazalisha
vitu vingi sana duniani, hata sehemu ya teknolojia tunaipata kutoka kwa
wahindi, sasa swalia la kujiuliza kwanini wao, kwanini na sisi tusijenge moyo wa uzalendo wa
kujituma?
Asikwambie mtu kama
utajituma kwa bidii na nguvu, akili za muda wako mwingi ni lazima utafikia
kilele cha mafanikio.
Acha utegemezi, acha
kuzembea unapokuwa kazini au kwenye mihangaiko yako ya kila siku, inawezekana
kufikia mafanikio kikubwa ni swala ma muda, na muda bila kujituma ni sawa na
mwanafunzi kuomba Mungu afaulu mtihani wakati hataki kujisomea wakati huo
vitabu vitakativu vinatuambia “ishikeni sana elimu msiiache iende zake”
Tafakari na fanya
mabadiliko kuanzia hapo ulipo, kwani hujachelewa.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:@mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U