Ni
Jumapili njema kabis machoni pa Mungu, nimepata kibali cha kuweza kuendelea
kutumia pumzi yake Mungu bila malipo yoyote yale. Ni jambo la kuimshukuru Mungu
kwa upendo wake nwa kweli kabisa.
Mada
yangu ya leo inajikita kwa mtu ambaye amekuwa akiachwa mara kwa mara na kila mpenzi anayekuwa naye. Zipo
sababu nyingi sana ambazo zinachangia watu kuachwa na kila mpenzi anayekutana,
baadhi ya sababu hizo ni:
NYOTA HAZIENDANI
Watu
wengine wanashinda kung’amua kuwa ili mapenzi yaweze kudumu bila kuwa na mizozo
mikubwa mikubwa wakati mwingine lazima ufahamu kuwa kuna ishu ya nyota kushabiana
au kutofautiana sasa kama mmekutana nyota zenu zinashabiana mtakuwa mnakorofishana
kwa muda kisha mnarudia vizuri sana na tena mpaka majirani wanashanga kwa
sababu tu waliamini kuwa ilikuwa ni mwisho wa penzi lenu kutokana na jinsi
mlivyorumbana juzi.
Unaweza
kukuta mtu akawa na mpenzi ambaye kila siku ugomvi, matusi, maneno na
vinginevyo haviishi kila kukicha lakini pia mtu huyo huyo anaweza akapata
mpenzi mwingine ambaye wakawa kama marafiki sehemu zote wanaongozana,
wanacheka, wanafurahia pamoja wakifika sehemu ya mapenzi wanakuwa wapenzi haimaanishi
kuwa wao hawagombani, la hasaha! wanagombana sana ila damu zao zimelandana.
Huu
ni ukweli unakuta mwenzio ana nyota ya moto alafu wewe una nyota ya maji katika
hali ya kawaida vitu hivi viwili havipatani, unadhani nini kitatokea kama sio
kushindana. nakupa mfano wa watu wawili
ambao walikuwa wanachuana vikali kwenye uchaguzi wa 2015.
Mh. Dkt. Rais JPM na ndugu Lowasa walikuwa kwenye nyota
mbili ambazo zote zina nguvu kwa mujibu wa Mnajimu wa Mambo ya Nyota, Maalim
Yahaya Hussein ambaye nilizungumza Nnilibahatika kuzungumza naye kabla ya
uchaguzi kumalizika, alidai nyota zao wagombea zilikuwa kali sana kiasi cha
kuwa na mvutano mkubwa hasa kama ambavyo kila mtu alishuhudia.
Vivyo
hivyo kwenye mapenzi kama nyota zenu hazirandani basi ujue migongano na
mapigano yatakuwa ni ya mara kwa mara baina yenu, kwa sababu tu mlikoseana
katika kuchaguana.
Usikose sehemu
inayofuatia kesho, muda kama huu. Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea
ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U