Habari mpenzi msomaji, nikualike tena kwa upendo wa dhati
kabisa katika somo letu linalojieleza hapo juu. Kupata nafasi hii ya kukupatia
somo haimanishi mimi ni bora kuliko wewe, la hasha ila wewe ni bora zaidi
kuliko mimi.
Dhamila ya somo tajwa nikukufanya ubadilike katika
mtazamo mzima wa kufikiri na kuamua katika maisha yako.
Leo hii wanafunzi yoyote ambaye anasoma ukimuuliza swali,
je, unasoma ili iweje?
Bila shaka majibu ya walio wengi watakwambia, mimi nataka
kuwa mwalimu, mimi nataka kufanya kazi benki, mimi nataka kuwa rubani, ni sawa!
lakini, je, masomo au elimu anayoisoma moja kwa moja inampeleka kuwa rubani,
mwalimu, askari, mwandishi, mwanamuziki na fani zingine? Utakuta hamna.
Watu wengi wanaamini baada ya masomo kuna ajira siyo
KUJIAJIRI, wengi wanaamini wakimaliza chuo kwa masomo au mchepuo aliochukua
basi atapata kazi fasta lakini kwenye uhalisia wa maisha haiko hivyo.
Somo la leo likubadilishe, uwaze namna ya kujiajiria na
siyo kuajiriwa, hata kama una ndugu yako unamsomesha,someshe kujiajiria na si
kuajiriwa, kwa kwa wanachuo hao ninaowaona baada ya kuhitimu vyuo mbalimbali
sioni ajira zao zinazoweza kukidhi wingi wao.
Bila KUFIKIRIA, KUSOMA AU KUSOMESHA mwanao au mpenzi wako
kwa lengo la kuja kujiajiria basi kila siku utaendelea kulalamika kuwa serikali
haijatoa ajira mpya.
Serikali haifanyi kazi, kwa sababu wananchi wahitimu
wanazurura hovyo mitaani na vyeti vyao wakisaka kazi.
Sina elimu kubwa sana ya kuajiriwa ila ni elimu kubwa
zaidi ya kujiajiri.
Kuna wakati nauchulia vibaya mfumo mzima wa elimu yetu
kwa sababu tu ni kama unampotezea mtu malengo yake, muda na mambo mengine,
kwani mwanafunzi anasoma akijua anakuja kuajiriwa.
Katika uhalisia hizo ajira ambazo unazifikiria hazipo, na
ni ujinga kusoma ukiamini utaajiriwa na kupata maisha mazuri.
Kama una mtazamo huo, umeula wa chuya, katika uhalisia wa
maisha nje ya shule ni tofauti sana. Kuna kuzunguka na vyeti weeee na kazi
hakuna, kuna kuombwa rushwa za pesa na ngono, kuna upungufu wa ajira zenyewe.
Lakini kama mfumo ungekuwa unakuandaa kujiajiri bila
shaka kila mtu angekula mazao yake.
Fikiri zaidi kuhusu kujiajiri hata kama uko kwenye ajira,
pamoja na kwamba haiwezekani wote tukajiajiri lakini wewe ambaye umebahatika
kupata sumu ya kujiajiri basi fanya hivyo.
Msomeshe mwanao kwa kile anachokipenda, mtengenezee
mazingira ya kujiajiri, kuwa mzalishaji wa bidhaa ili akimaliza masomo yake
ajue anachofanya.
Kama unasoma, soma kwa kujiajiria na siyo kukalia
vimbweta kwa kuamini kuwa unasoma ukaajiriwe.
Ninachoamini mabadiliko yanaanza na wewe muhusika kwa
kujitambua kisha kufanya yale ambayo unahisi yanastahili kufanywa na wewe au
mtu yeyote anayejitambua.
Acha kuifanya akili yako kuwa tegemezi, akili yako
kuiegemeza kwenye kuajiriwa. Kwani huwezi kufanya japo jambo dogo la kujiajiria
angalau kwa kufungua kibanda cha pipi, machungwa au genge kwa sababu tu una
amini una tuzo unayostahili baada yakuhitimu chuo.
Hii siyo nchi ya hivyo, hata huko kwingine ambako unahisi
kuna ajira kibao, si kweli, bali hata wao wanaangaika ila kwa kuwa mfumo wao
wameufanya kujiajiri kwa mhusika na ndiyo maana leo hii tunatumia vifaa, huduma
za wenzetu.
Kwa
Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya
Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na.
0657486745.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au
tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na:M&U.