NILIPOISHIA…
Maiko akanipa hongera kwa kujifungua salama, kiukweli
ni kama alinitonesha kidonda changu ila kwa kuwa alikuwa ameomba msamaha na
kunitaka tukaishi naye wote sikuwa na nafasi ya kufikiria yale maumivu ya
awali.
ENDELEA…
Nilijiona mpya kabisa katika maisha yangu,
nikaendelea kuishi kwao Maiko akiwa na chumba chake kimoja tu, pembeni kukiwa
na ndugu zake kibao, kwa ujumla familia ya Maiko yote ilikuwa pale kwenye
nyumba ya familia. Bila shaka unafahamu mazingira ya maisha ya nyumba za uswahili.
Maiko alikuwa anafanya kazi kwenye ofisi
moja kama kibarua, hakuwa ameajiriwa hivyo hakuwa na kipato cha uhakika
saaaana, lakini alivyokuja kule kijijini alijigamba kana kwamba anakazi nzuri
yenye kuboresha maisha yake na yako na kwa jinsi alivyokuwa amejipigilia
haikuwa rahisi kumshitukia na kumuona mjanjamjanja na kwa mwanamke yoyote
ilikuwa rahisi kuingia kwenye himaya yake.
Kutoka na hali duni ya kifedha ya mume
wangu tusiye na ndoa nilikubaliana na hali ile ya kula wakati mwingine mlo
mmoja au siku inapita labda usiku ndiyo unabangaiza. Na haikuwa hali ngeni
kwangu kwa sababu hata kijijini kwetu nimepitia hali hiyo, hivyo haikunisumbua
sana.
Kwa hiyo nikawa naishi na maisha hayo hivyohivyo
kwa shida, huku mume wangu naye akiendelea kuninyanyasa, aachi pesa yakutosha
ya matumizi, kwa mfano mtu anakuachia shilingi 500 wakati anafahamu kabisa una
mtoto unanyonyesha na unatakiwa kula chakula kingi cha kushiba ili kupata
maziwa.
Baada ya muda kupita ndipo hapo
nilivyoanza kujionea vimbwanga vya familia ile , nadhani awali walikuwa
ananikaribisha tu kama mgeni, mara visa
vikaanza kwa wadogo zake, unaweza ukapangiwa zamu ya kufagia mwezi mzima wao
wakiwa wametulia tuli. Kwa kuwa nilikuwa ni muolewaji sikupenda kuonesha dharau
nilivumilia lakini moyoni niliumia.
Ikafika sehemu hata ile pesa kidogo
ninayoaachiwa na Maiko , mama yake mzazi anaitaka, anakuja kuomba nimuazime,
nikimwambia mama leo sina pesa, anasema ninatumia tu hovyo pesa za mwanaye
wakati hata mtoto niliyenaye siyo damu
yao.
Nilistuka kusikia mama mkwe wangu anasema
hivyo, “Mama mbona yamekuwa makubwa mama yangu, kweli sina pesa mama,”
nilimwambia hivyo.
Cha ajabu mama mkwe alinikata jicho hilo
ambalo sijawahi kukutana nalo katika maisha yangu, ama kweli kuwa uyaone. Mama alininisonya
na kuondoka zake.
Nini
kilifuatia baada ya kukatwa jicho la husuda na mama mkwe wake?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U