Vipo vyanzo vingi sana vya
mtaji ambavyo vinaweza kukusaidia wewe mjasiriamali mdogo mdogo kutoka hapo
ulipo na kufikia mafanikio unayoyawaza.
Ingawa sehemu kubwa ya mtu
au watu wanaotaka kuwa wajasiriamali, swali lao kubwa na gumu huwa ni namna gani anaweza kupata mtaji wa kuanzisha
biashara.
Kiukweli kama unataka kuwa
mjasiriamali unapaswa uthubutu na kuumiza sana akili namna ya kupata mtaji.
Vyanzo vya mtaji inaweza
kuwa ni;
Hisa za mmiliki
Kama umekuwa na tabia ya
kuwekeza na umewekeza kwa muda sasa
unaweza kuchukua sehemu ya hisa zako nakuzifanya kuwa mtaji wa biashara
inategemeana na aina ya biashara unayotaka kuifanya.
Mikopo
Kukopa kwa ajili ya
kufanya biashara si jambo baya kama utakuwa umejipanga vilivyo katika kutimiza
na kuifanyika mkopo huo wa fedha au vitu, ingawa wengi sana wanaema sio nzuri
kwasababu wanakopa kwenda kufanya vitu vya starehe na sio walichokikusudia.
kudunduliza kidogo kidogo.
Mtaji mzuri ni ule wa
kuutafuta wewe mwenyewe kwa kukusanya fedha kidogo kidogo ‘kududuliza’ unaweza
kuanza kwa kutengeneza ‘kiboksi bubu’ na ukawa unaweka japo mia mbili kwa siku
baada ya muda utajikuta una pesa nyingi ambazo zitakuwezesha kuanza biashara.
Kama mtaji utakuwa uliudunduliza mwenyewe unakuwa na uchungu sana pia itakufanya
kuwa makini na kuongeza mbinu za kuulinda mtaji huo ili usiporomoke kiaina
aina.
Benki
Hili halina utofauti sana
na mikopo, karibu benki zote huwa na vitengo vidogo vidogo kwa ajili ya
kushughulikia wafanya biashara wadogo wadogo, ila ni lazima uwe na vigezo ili
kuweza kukidhi kuwa mkopwaji ni lazima uwe na; mchanganuo wa biashara yako (Busness
Plan), udhamini na vinginevyo. Na mwisho ni lazima urejeshe riba na mkopo
uliopewa.
Familia au rafiki
Mtaji pia unaweza kuupata
kwa kusaidiwa na familia au rafiki yako, ili waweze kukusaidia ni lazima
uwaonyeshe ni kwa namna gani umedhamilia na unaweza kuimudu biashara hiyo, kwa
kufanya hivyo ni rahisi sana kukusaidia mtaji wa kuanzia.
Taasisi za serikali
Katika sekta nyingi za
serikali kuna vitengo maalumu kwa ajili ya kutoa mikopo kwa vikundi mbalimbali
vikiwemo vya ujasiriamali na vya vijana.
Mashirikia yasiyo ya kiserikali
Hali kadhalika hata
mashiriki yasiyo ya kiserikali nayo yanahuduma ya kutoa mikopo kwa vikundia au
wajasiriamali wadogo, kikubwa ni kujua namna gani ya kuweza kupata mkopo huo,
usiogope masharti au muda mrefu wa kufuatilia.
Misaada
Hii ni sehemu pia ya
kuweza kukufanya ukapata mtaji kwa ajili ya kuanzisha biashara yako, msaada
mara nyingi huwa hauna mrejesho, ukipewa umepewa.
Vyanzo vingine
Vipo vyanzo vingi kama
nilivyosema awali, vingine ni kama shamba, aridhi, miti, mawe na kadhalika.
Angalizo sehemu kubwa ya Watanzania
wengi hawapendi kusumbukia au kujihangaisha ili kuhakikisha anatimiza ndoto
yake, mitaji iko mingi unachotakiwa ni kuifuatilia ilikuweza kujua ni mikakati
ipi unapaswa kuifuata iliufanikishe.
Kwa uzembe huo ndiyo maana
mafisadi wengi wanaibuka kila siku kwa kuanzisha taasisi, vikundi na makapuni
hewa ili kupiga hela hizo.
Zinduka, funguka anza mwanzo mpya.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa.
Na.M&U