Karibu tena siku hii kwa
ajili ya elimu ya ujasiriamali, elimu ambayo inatuma kujifunza na kuelewa namna
ya kukabiliana na changamoto za maisha ya kila siku.
Somo la leo linahusu
mfanyabiashara mmoja kuwa katika kipindi kigumu lakini kwa mfanyabiashara
mwingine kwake ni kipindi kizuri na cha neema kwa yeye kutengeneza kufanya biashara
na kutengeneza pesa nyingi zaidi.
Ni kweli majira
yamegawanyika katika sehemu kuu mbili:Masika na kiangazi. Kwa wafanyabiashara
walio wengi hutumia majira ya kiangazi kukusanya baadhi ya nafaka kama mahindi,
mpunga mtama na nyinginezo ili ukiwadia muda wa masika basi kwao ukitumia kwa
ajili ya kufanya biashara wanayoamini ina faida nzuri kwani watu wengi huwa
wanaogopa kuwekeza kwa kuhofia kupata hasara.
Wakulima wenyewe kipindi
cha masika hukitumia kwa ajili ya kupanda sana mazao kama mpungu, maharage,
mahindi na mengineyo ili kikifiika kiangazi basi afanye biashara nzuri.
Lakini kwa baadhi ya
wakulima inapofika kipindi cha masika kuna wengine wanaokimbia kwa kuacha kulima
kwa sababu mvua zinakuwa ni nyingi na zenye kuzalisha wadudu wengi wanaoshambulia
mazao hivyo ni mara chache sana kuweza kuvuna mazao yao katika hali inayotakiwa
hivyo wanaona kusimama na kusubiri muda ukifika ndipo waanze tna mikakati ya
kulima.
Lakini baadhi ya wakulima
wao hujifunga kibwebwe kwa kuhakikisha wanakitumia vizuri kipindi cha masika
kwani, wanaohitaji bidhaa ni wengi na haipatikani na kwa wanaopatikana ni wale
ambao wamejitoa muhanga kwa ajili ya kutumia kipindi hicho kutengezeza pesa.
Kwa mfano mkulima
anayelima zao la nyanya uogopa sana kulima zao hilo kwa sababu linahitaji
umakini, uvumilivu na uangalizi wa hali ya juu sana ikiwemo dawa za kuondoa
ukungu na wadudu hivyo kuifuatia mahitaji hayo wakulima wengine hushidwa kumudu
gharama za mahitaji hayo hivyo hujikuta wakiamua kumwaga manyanga chini.
Kitendo cha baadhi ya wakulima
kumwaga manyanga chini basi zao la nyanya uadimika na kupanda bei.
Lakini kwa mfanyabiashara
au mkulima mjanja hutumia nafasi hiyo kutengeneza pesa kwa wingi kwani huwekeza
katika madawa na huduma zingine lakini pia kulima zao hilo la nyanya kwa
umakini zaidi ili aisiingie hasara na hufanya hivyo kwa kujua kama atatumia
muda wake mwingi kulitunza ao hilo vizuri basi kikifika kipindi cha mavuno
atafanya biashara nzuri, kubwa na kwa bei anayotaka kutokana na wahitaji kuwa
wengi huku wengine wakipandishiana bei wao kwa wao.
Na ndivyo vivyo kwa
mjasirimali kwenye kiu na nia ya kuthubutu ili kufikia mafanikio kwa hutumia
mbinu zile zile kama alizotumia mkulima mwenye kufanya kazi ya kilimo katika
kipindi kigumu cha wadudu wengi ambao huaribu mazao.
Mjasiriamali mwenye kiu ya
kufikia malengo yake yuko tayari kujitoa au kujitosa kwa kufanya jambo ambalo
ni hatari kwa biashara yake hasa katika kipindi ambacho wengine ukiogopa ila
yeye ukitumia kuhakikisha anapata mafanikio.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U