NILIPOISHIA…
Cha ajabu mama mkwe alinikata jicho hilo
ambalo sijawahi kukutana nalo katika maisha yangu, ama kweli kuwa uyaone. Mama
alininisonya na kuondoka zake.
ENDELEA…
Nilibaki nikishangaa sana mama kwa kitendo
kile nilijiuliza nini kikubwa ambacho nimemkosea mama yangu jamani, au tatizo
langu ni kumwambia kuwa sina pesa ndiyo ameamua kunitukana na kuniangalia jicho
la husuda kiasi kile utadhani labda mimi ni mke mwenzake.
Niliingia ndani na kuanza kulia, nililia
sana, nilifikiria mambo mengi sana, siku hiyo hata sikuhisi hamu ya kula kitu
chochote zaidi ya kulia.
Nilijiuliza sana nini kinamfanya mama
aseme kuwa mtoto niliyezaa na Maiko siyo damu yao, ana maana gani? Je, inawezekana
Maiko ndivyo alivyomwambia mama yake au familia nzima ndivyo huwa wananijadili
hivyo nikiwa sipo nyumbani.
Nilifikia sehemu kama mwandamu nikaanza
kuhisi labda pengine Maiko pale siyo kwao, kapanga tu na anatembea na mama
mwenye nyumba, maana siyo kwa mchambo ule.
Nilifikiria mambo mengi sana, tangu
nilivyojitunza ili kupata mume sahihi, namna ambavyo Maiko alikuja kunipata kwa
kujifanya ni muungwana kumbe tapeli wa mapenzi, nikaingia kwenye kumi na nane
zake, akatoa usichana wangu, akanipa ujauzito, akanitelekeza, nikateseka na
ujauzito wa mwanangu kwa miezi yote huku nikiishi kwa shidashida,.
Nikakumbuka pia masimango ya baba wa kambo kwa
mama yangu dhidi yangu, namna ambavyo nikajifunguliwa porini nikiwa na mama
yangu mzazi.
Machozi yalianza kunilengalenga tena na
kujikuta nikianza kulia kwa kwikwi ila kilio chenye uchungu na hasira ndani
yake. Niliendelea kulia hadi muda wa Maiko wa kutoka kazini, akawa amerudi na
kunikuta nalia.
Nini
kilifuatia, baada ya Maiko kumkuta mkewe
analia?
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi,
Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS
au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com,
Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U