Monday, January 16, 2017

Published 1/16/2017 04:00:00 PM by

NIMEAMUA KUJIUZA!-11



NIMEAMUA KUJIUZA!-10

NILIPOISHIA…..
Miezi mitatu ilipita bila mtoto kupewa jina, akaendelea kunisumbua sana ikiwa mtoto ni wa kulialia tu mara kuugua, nikaamua kwenda tena kule center kwa ajili ya kumtafuta Maiko kwenye simu.

SONGA NAMI……..
Muda ulipita mtoto akiendelea kunisumbua, huku mama ana majirani wakidai ilikuwa ni lazima baba yake mzazi ampe jina ndipo atakaponyamaza.

Niliumia sana kwa hali hiyo kwani sikuwa natamani kabisa kumuona Maiko maishani mwangu, nilitamani kama ingewezekana kumpa jina mtoto wake hata kwa njia ya simu au SMS basi ningeomba afanya hivyo lakini haikuwezekana.

Niliendelea kufikiria namna ya kukabiliana na hilo bila kufahamu, nikiwa nimechoka kabisa kufikiria namna ya kumpata Maiko ili aje ampe jina mwanaye nilishangaa kupokea ujumbe ambao ulikuwa ni wasamahani sana kuhusiana na kile kilichotokea dhidi yangu na Maiko.
 
Ndani ya bahasha ile kulikuwa na nauli pia ya kutoka kijijini hadi mjini, mjini hadi nyumbani kwa wazazi wake Maiko ambao walikuwa kuwa wanaishi wilayani Ifaraka Mkoa wa Morogoro.

Sikuwa na furaha kwa samahani na pesa ile aliyonitumia eti, kasikia nimejifungua hivyo anataka akamuone mtoto wake pamoja na kumpa jina, kweli Maiko ni mwanaume wa ajabu, katili sana, anajua ni kwa jinsi gani mimi nimeangaika na mtoto wangu kuanzia mimba hadi kujifungua, na mbaya zaidi nimejifungulia porini, hadi siku hiyo mtoto wangu hakuwa amepewa chanzo wala dawa ya aina yoyote ile kwa sababu sina nauli ya kwenda zahanati.

Nilimsimulia mama kila kitu kilichotokea  na uchungu nilionao kuhusu Maiko, mama akanisihi sana na kunishauri ni bora niende kwa mzazi mwenzangu kwani pengine amejirekebisha, matatizo ya kwenye mapenzi huwa yapo tu hata yeye ana mambo mengi yanayomsibu na mumewe sema mengine huwa haniambii kama mtoto.
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Je, Kecho alikubaliana na ushauri wa mama yake kuwa aende Morogoro kwa mzazi mwenziye. Pia unaweza kupata mikasa huu kwa kujiunga na M&U SMS kila siku kupitia Na.0657486745.
Na.M&U

@@@

NIMEAMUA KUJIUZA!-11
 
NILIPOISHIA…
Mama akanisihi sana na kunishauri ni bora niende kwa mzazi mwenzangu kwani pengine amejirekebisha, matatizo ya kwenye mapenzi huwa yapo tu hata yeye ana mambo mengi yanayomsibu na mumewe sema mengine huwa haniambii kama mtoto.

SONGA NAMI…
Nilimkatalia mama yangu, nikageuka mbogo, nikaona mama amebadilika na kuwa mnyonge sana kisha akaanza kulia na kuniambia.
“Mwanangu Kecho nimekuwa nikigombana na baba yako kwa sababu yako wewe, anadai kuwa kwanza siyo mwanaye wa kuzaa alafu tena na wewe umezaliwa nyumbani.

Wewe ni mzigo kwake na wewe tena unamuongezea mzigo mwingine, kuna wakati baba yako anataaka kuniacha akidaia hawezi kuendelea kulea mwanamke mzima kama wewe ambaye unaweza kabisa kuolewa, mwanangu ni bora uende tu kwa mzazi mwenziyo ili unipunguzie matatizo mama, unadhani kama  baba yako ataamua kuniacha nitakuwa mgeni wa nani mimi, nani ataniona na utu uzima huu?.

“Sikupenda kukuambia maneno haya mwanangu lakini sina budi, imebidi nikwambie tu mama, nakupenda mwanangu, wewe nenda Mungu atakutangulia, wanaume wote wana matatizo, mimi mwenyewe naishi na baba yako kwa tabu sana, ila sina jinsi kwa kuwa maji niliyavulia nguo acha niyaoge, sinilichagua kuolewa acha niendelee kuishi naye.

“Kuna wakati namkumbuka sana baba yako kwani alikuwa ni mwanaume aliyenipenda na kuniheshimu sana, pamoja na kuwa na kipato duni lakini tulifurahia penzi letu na hata maisha yetu kwa ujumla ila siyo kwa baba huyu,’’alisema mama huku akiendelea kulia.
 
Niliumia sana, nikaanza kulia na mimi, baadaye nikajikaza na kufuta machozi kisha nikaanza kumbembeleza mama yangu na kumwahidi kuwa nitaenda Morogoro kwao Maiko na nitajitahidi kuvumilia kila changamoto kama ambavyo yeye amekuwa akivumilia kwa baba wa kambo.

Nilimchukia sana baba wa kambo moyoni mwangu, sikujua kama mimi nimekuwa mateso na msimango kwa mama yangu, nilianza kumfikiria Maiko na kuona kumbe wanaume wote ni makatili sana, basi nilimuahidi mama kuwa niko tayari kwenda.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Usikose kesho katika mkasa huu wa kweli ambao umemkuta msichana Kecho. Pia unaweza kupata mikasa huu kwa kujiunga na M&U SMS kila siku kupitia Na.0657486745.
Na.M&U
      edit