Thursday, January 12, 2017

Published 1/12/2017 12:00:00 PM by

ETI, NIKIPATA UJAUZITO BABA ATARUHUSU NIOLEWE!



Jina langu ni Zuhura ni binti wa miaka 19, ni mwanachuo ambatye natarajia kumaliza ngazi ya cheti hivi karibuni kwenye moja ya chuo kilichopo jijini Mbeya. 

Niko kwenye uhusiano wa mapenzi na mchumba wangu kwa miaka minne sasa, yeye ana miaka 24 na ndiye aliyeniingiza kwenye utamu wa mapenzi.
 
Mimi ni mtoto pekee katika uzao wa mama na baba yangu, kwa sasa naishi na bibi na babu, kwa sababu baba yangu mzazi huwa anaishi nje ya nchi.

Baba alitamani sana niende nje nikakae naye pamoja na kusomea huko lakini nilikataa, baba alikubali na kunisihi nisifanye mzaha katika maisha yangu na ikitokea nikafanya basi atanichukia sana.

Baada ya kusikia nategemea kumaliza awamu ya kwanza ya masomo hivi karibuni baba ameanza kufanya maandalizi ya mimi kwenda nje ya nchi. Kiukweli mimi siko tayari kuondoka Bongo kwani sitaki kulikosa penzi la mchumba wangu, niko tayari kuolewa na yeye, na hata yeye karidhia. 

Ninachokifiria kwa sasa ni kubeba ujauzito wa mchumba wangu ili wazazi wangu wakubali kuniozesha kirahisi na nisiende nje ya nchi.
Ungekuwa wewe ndiye mimi ungefanyaje, au unanishauri nini kwa kile ninachokifikiria?

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa


Na.M&U

      edit