Ni nadra Sana kuishi
katika dunia hii bila kuumizwa katika mahusiano hasa ya mapenzi, unaweza
kuumizwa kwa aina nyingi, yawezekana ukaumizwa kwa kuachwa na mtu ambaye
ulimpenda sana au kuumizwa kwa kutendwa vyovyote vile na mpenzi wako.
Mtu mmoja aliamini yeye ni
shujaa na shupavu wa mapenzi kwa sababu hakuwahi kuumizwa katika uhusiano wake
na aliamini hakuna mwanamke chini ya jua ambaye angeweze kumsumbua, kumuumiza,
kumtesa na kumnyong’onyesha kiakili au kiafya kwa sababu ya penzi lake.
Lakini mwisho wa siku
jamaa akakutana na mwanamke ambaye ana watoto na jamaa kampenda mwanamke yule
kuliko alivyowahi kupenda awali.
Kwa sababu maumivu ya
mapenzi yapo tu, hata kama siyo ujanani basi utuuzimani, leo jamaa analalamika
na kusema kuwa: “Ninaumia, ninateseka, nimedhoofika kiafya kwasababu ya
mwanamke huyu, mwanamke ninaye mpenda, nimegeuka kipofu, zuzu, nimeisha tukanwa
sana, nimepigwa sana lakini kutoka moyoni mwangu nampenda sana, sina amani
maishani mwangu bila penzi lake, nimejaribu kumwambia juu ya hisia zangu kwake
hanielewi, nimejaribu kumuonesha namna navyompenda lakini bado hajanipa nafasi.
“Sina raha na maisha haya,
najiona kama mtu niliye nyikani, sina maji, wala chakula, sina nguvu mwilini
japo za kujivuta hatua moja mbele. Sili nikashiba kwa sababu yake, silali
jamani, kisa kikiwa ni penzi lake, hata ule ununda wangu wa kwenye mapenzi
siuoni tena, niko radhi kwa chochote kile ila siyo kumkosa mwanamke huyo.”
Hayo ndiyo mapenzi bwana,
hayana cha komandoo, staa, waziri, mfanyabiashara, maskini, tajiri, mlemavu au
msomi, kama yakikukorea yamekukolea tu.
Tukutane kesho katika mada nyingine yenye elimu
zaidi juu ya mapenzi. Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za
Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge
na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 au 0679979785.
Na.M&U