Saturday, January 7, 2017

Published 1/07/2017 04:00:00 PM by

MIMI NI MJANE, KUNA KIJANA NIMEMPENDA JE, KUNA TATIZO NIKIMWAMBIA?



Mimi ni mama mjane ambaye mume wangu alifariki dunia takribani miaka 3 iliyopita kwa tatizo la mshtuko wa moyo. Ni mama wa miaka 42 na nina watoto wanne.
 
Nimekuwa nikiishi katika upweke kwa muda mrefu sana na hata nilipoppata mtu wa kunifariji hakuwa na mapenzi ya kweli zaidi ya kunitumia na kuchikichia na kunifanya niendelee kutamani na kukumbuka uwepo wa marehemu mume wangu.



Baada ya kukaa kwa muda mrefu nikiwa na upweke wangu hatimaye nimempata kijana wa miaka 33 (MALIOO) ambaye yuko nje ya nchi. Ananipenda sana na mimi ninampenda na yuko tayari kuishi na mimi, ameshanitumia baadhi ya pesa kwa ajili ya kuanzisha mradi wa Bongo na hata pesa ya matumizi amekuwa akinipatia.

Nilimuuliza kwa nini ameamua kuwa na uhusiano na mimi mtu mzima ambaye ninamzidi miaka 9, alisema kuwa utu uzima siyo tatizo kwake ni dawa kwani anaamini kuwa mabinti hawana uchungu na maisha hawawezi kutunza na kuendeleza mali zake ambazo zipo hapa nchini.
Kiukweli nampenda lakini wasiwasi wangu ni utofauti wa miaka yetu naona kama jamii itanishangaa na kunisema sana.
Naomba ushauri wako, ili na mimi niondokane na hili dukuduku nililonalo moyoni mwangu.
 
Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na.M&U
      edit