Wednesday, January 11, 2017

Published 1/11/2017 04:00:00 PM by

NDANI YA AKILI KUNA AKILI!



Kama ulikuwa hujawahi kufikiria hili basi litambue na anza kuifanyia kazi akili ya ndani ya akili.
Akili hiyo ndiyo inayokutenganisha wewe na wingine, akili ambayo ikifunguka, utakuwa ushajijua wewe ni nani, una uwezo upi katika hii dunia.

Akili hiyo ndiyo ambayo inaweza kukuongoza katika kuelekea kwenye mafanikio. Kwani ni akili yenye ziada ya katika kufikiria.

UNAWEZAJE KUIFAHAMU AKILI HIYO?

Ni lazima ukae  chini na kujifikiria, je, ulivyo hivyo ndivyo ulivyo, na ndivyo unavyostahili kuwa. Kama ndiyo basi sawa lakini kama sivyo, jiulize kwa nini?

JICHAMBUE

Ukishaweza kupata jibu kwa nini, kisha jichambue kimoja kimoja, kuanzia unyayo hadi utosi huku ulijiuliza umewezaje kutumia akili yako katika kutimiza ndoto zako

AKILI YAKO, UMEITUMIA KWA ASILIMIA NGAPI?

Kwa kuwa vitu vingi huanzia asilimia 0  hadi 100 basi.hata akili ina asilimia 100. Lakini ulishawahi kujiuliza umetumia asilimia ngapi ya akili uliyonayo?  Ukijiuliza sana utagundua umetumia asilimia ndogo sana ya akili hiyo, pengine tangu umezaliwa hadi ulipo umetumia asilimia 25 tu ya akili yako, 75 zilizobako hazijawahi kutumika wala kugiswa, sasa jiulize, kama hujazitumia ziliwekwa za nini? Na umezibakiza za nini?

Wenzako waliofanikiwa wametumia sehwmu kubwa ya akili yao katika kufikiria zaidi, katika kuwaza kutafuta majibu ya changamoto na magumu wanayoyapitia na mwisho wa siku wakashinda.

Ushindi wowote hauji bila kufanya mazoezi, bila kushindana. Yafanye matatizo yako kuwa mashindani wako, matatizo yanapokuja usiyachukie, bali jiulize kwa nini tatizo hilo limekuja kwako?   Ukipata jibu la kwa nini limekuja kwako, basi tafuta jibu la nini ufanye au kifanyike kutatua changamoto hiyo hapo ndipo utakapoibuka kuwa mshindi katika matatizo yanayokikabili yote yaliyo ndani ya uwezo wa kibinadamu.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745. 

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na.M&U
      edit