Ama kweli kwenye miti miti mingi hakuna wajenzi!
Nikiwa ndiyo nimeanza kuwa binti kigoli nilifanikiwa kukutana na kijana mmoja nakuanzisha
mahusiano ya mapenzi, kijana huyo alikuwa ni Mkristo na mimi nikiwa ni
Muislamu.
Tulidumu kwa muda mrefu kwenye mapenzi yetu hadi
tukafanikiwa kupata mtoto wa kike. Yule kijana aliniahid kunioa ila hakufanya
hivyo kwa madai kuwa alikatazwa na ndugu zake asibadili dini kwa ajili yangu.
Niliamua kuachana naye na kuanza maisha yangu mapya
ingawa baadaye Yule kijana alikuja akamuiba mtoto wake. Baada ya miaka mitatu kupita
nikapata mwanaume ambaye ni Mkristo mwenzangu na yuko tayari kunioa.
Kilichonishangaza kwa hivi karibuni ni kitendo cha
mzazi mwenzangu kuja na kusema kuwa yuko tayari kubadili dini ili tufunge ndoa.
Kumpenda bado nampenda sana lazizi wangu na niko
tayari kuolewa naye na sipendi kuwa na watoto wa baba mbalimbali.
Swali langu
linalonisumbua kichwa vipi kwa mchumba ambaye nilikuwa nimempata? Je,
nikimuacha si nitakuwa nimemuumiza sana kijana wa watu. Hapo tu ndiyo pagumu
katika mtihani wangu nilio nao, nahitaji mawazo yenu wadau wa M&U.
Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa
Na.M&U