Monday, January 23, 2017

Published 1/23/2017 06:00:00 PM by

BAADA YA SALAMU NI MIZINGA, INAWAPONZA SANA KINADADA



Tumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutukutanisha tena siku nyingine ya leo, kabla ya yote naomba kuwapongeza na kuwashukuru Watanzania kwa upendo wa dhati na wa kweli kwa kudumisha amani ya nchi yetu katika kipindi kigumu tulichokuwa nacho cha uchaguzi mkuu.
Mada yangu ya leo inahusu moja ya tabia inayowaponza kina dada au wanawake ya kupiga mizinga kwa wapenzi wao na hata wasio wapenzi wao.
 
Mmoja wa wasomaji wangu alinilalamikia kuwa yeye amekumbwa na kisanga hiki baada ya kupigwa mizinga na mwanamke ambaye hana uhusiano naye wa kimapenzi zaidi ya kukutana kweye mitandao ya kijamii na kuanza kuwasiliana.

Tumsikie
Hii mitandao ina mambo sana, nilikutana na mdada mmoja tukafahamiana na kubadilisha mawasiliano, nilijua tutakuwa tunazungumza mambo ya kawaida tu lakini tulivyozidi kuzoeana ikawa kila nikimpigia baada ya kubipu ni salamu kisha mizinga.
“Dah! Wangu nimepinda mbaya, kama vipi nitoe hata twenti (20000)”.
Kama ikitokea nikamwambia sina pesa basi ataomba nimrushie vocha na tabia hii si mara moja, imezidi sana ndiyo maana nimeamua kumuuliza mtaalam wa Maisha na Mapenzi.

Athari zake
Kwa tabia hiyo ya kupiga mizingi watu hovyo imewakuta ikiwagharimu wanawake wengi kuingia katika uhusiano usio rasmi.

Inakuaje
Unapozoea kupiga mizinga mtu ambaye huna uhusiano naye wowote ni sawa na kujirahisisha mwenyewe kwa jamaa huyo, wakati mwingine jamaa anaweza kuwa hana dhamira mbaya na wewe wala hajawahi kuchezwa na mshipa dhidi yako ila kwa mizinga yako itapelekea kujenga mazoea mengine zaidi ya hayo na unajikuta ukisaliti ndoa au uhusiano wako kirahisi.
 


Nililolibaini
Kuna baadhi ya wanawake wanaishi mjini kwa tabia hiyo ya mizinga ya vocha kama sio vocha basi pesa, wakati ukweli ni kwamba hawana uhusiano wa karibu sana na yule anayempiga mzinga.

Ushauri wangu
Wanawake muache tabia hii kwani haipendezi na wala wanaume hawaipendi ndiyo maana inawasukuma kujiingiza katika uhusiano kiholela na wanakuwa hawana mapenzi ya kweli zaidi ya kufidia mizinga ya pesa na vocha ulizokuwa ukimpiga na kiukweli mizinga hiyo inawaponza sana.

Kwa Ushauri Wa Mahusiano, Mada Za Mahaba, Hadithi, Machombezo, Mikasa Ya Kweli Ya Mapenzi Na Ujasiriamali. Jiunge na M&U SMS au M&U WhatsApp kupitia Na. 0657486745 AU 0679979785.

Pia tembelea www.miminauhusiano.blogspot.com, Insta:mimi_na_uhusiano au tembelea ukurasa wetu wa Mimi na Uhusiano kwenye Bonyeza Hapa

Na.M&U


      edit